Kumekucha, Msanii Nikki Mbishi aitwa na Baraza la Sanaa Tanzania ''BASATA'' kujieleza kuhusu maudhui na hatma ya wimbo wa ''I am sorry JK''
Wimbo huu pia uliwahi kujadiliwa hapa JF, soma
Msanii Nikki Mbishi amuomba msamaha Kikwete
Kuna mashairi anaimba
Kila taarifa ya habari leo JPM/
Pesa imepotea kimazingara David Blaine/
Waathirika hawaelewi juu ya mipango ya Bukoba/
Tetemeko wasije kula michango ya Msoga/
Tumekosa usitupe laana tucorrect/
Weka kando chama tuwe wana tuconnect/
Je, Rungu litampitia msanii huyu wa nyimbo za harakati?
Wimbo usikilize hapa...