Mtepetallah
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 230
- 131
Shusha mzigo huo
Mwenye link riwaya ya NJAMA naomba atupie hapaKumbe ipo siku nyingi?
Bora ww unaesubiri end.... maana utamu unakuja halafu unakatanasubiri nikiona neno end ndo nianze kuisoma. Plz siku ikiisha mniite
Kumbe ni hadithi za kutungwa napata tabu kusomaRIWAYA: Wimbo wa Gaidi
MTUNZI: Hussein Tuwa
SEHEMU YA PILI
Na ni kutokana na uhatari wa eneo lile ndipo watalebani waliojaa hila na shuku zisizo ukomo, walipoelekeza kuwa ndege zile za misaada ziangushie marobota makubwa ya chakula na madawa kwenye eneo lile, kisha ndege zitakazoangusha misaada ile zigeuzie huko huko angani na kwenda zake. Hakukuwa na ruhusa kabisa kutua pale kijijini wala sehemu yoyote ya eneo lile walilolidhibiti vilivyo, la Waziristan ya Kaskazini.
Ndege ya kwanza ilitokeza kutokea nyuma ya milima mingi iliyolizunguka eneo lile, na minong’ono ya viherehere ikazagaa miongoni mwa wanakijiji. Ndege ikazidi kukurubia huku ikizidi kushuka. Watalebani wengi wa shuku wakajizatiti kwa silaha makini wakiwa miongoni mwa wanakijiji ambao sasa waliwakusanya kuwafanya kama ngao zao dhidi ya shambulizi lolote kutoka kwenye ndege ile. Na hata pale walipoanza kujizatiti namna ile, ndege nyingine tatu zilioneka kutokeza juu ya vilele vya milima iliyolizunguka eneo lile, na dakika kumi baadaye marobota makubwa yalionekana kuanguka kutoka angani. Mayowe yalizagaa, wanakijiji wakazidi kujirudisha nyuma ili kuwa mbali na eneo lile la wazi lililokuwa likimulikwa kwa ile mioto kutoka pembe sita tofauti. Lakini muda si muda, maparashuti yakafunuka kutoka kwenye marobota yale makubwa, nayo yakaanza kushuka taratibu huku yakinesanesa hewani kwenye anga ile ya usiku. Wanakijiji na watalebani walijitahidi kwa kadiri walivyoweza kufuatilia ushukaji wake kwenye kiza cha usiku ule wenye mbalamwezi hafifu, lakini haikuwa rahisi. Marobota yalizidi kushuka, kila moja kwa uelekeo wake…kila moja likiwa na shehena muhimu kwa wanakijiji wa Dargar Mandi ndani yake…lakini pia juu ya kila mgongo wa robota la vyakula vile, kulikuwa kuna siri kubwa….
________________
Makomando wanne walishuka kwa maparashuti wakiwa wamelala juu ya migongo ya yale marobota makubwa ya chakula cha msaada yaliyokuwa yakiangushwa na ndege za msalaba mwekundu kwenye kile kijiji cha Dargar Mandi. Wote wanne walikuwa wamevaa nguo maalum za kuzamia mbizi majini bila ya kulowa.
Lengo lao lilikuwa ni moja tu. Kumkomboa mtanzania aliyenaswa ndani ya kijiji kile, akiwa ni mmoja wa wapiganaji wa Al-Qaeda aliyetajwa kutafutwa na FBI baada ya shambulizi la kutisha kwenye ubalozi wa Marekani jijini Dar mnamo mwaka 1998. Sasa ngome iliyosalia ya Taleban ilikuwa inawahifadhi baadhi ya wapiganaji wa Al-Qaeda waliobakia, yeye akiwemo, ilikuwa imezingirwa na majeshi ya ushirika wa Marekani na Pakistani. Upinzani wa Taleban ulikuwa unaelekea kushindwa, na wamarekani wakiingia ndani ya ngome ile hakutakuwa na garantii ya mtanzania yule kunusurika.
Isipokuwa kama atatolewa mle ngomeni kabla majeshi ya washirika hayajavamia.
Lakini kivipi?
Ndipo nafasi ilipojitokeza pale Taleban walipokubali wanakijiji waletewe vyakula vya msaada kwa njia ile.
Marobota yanatua kwa vishindo ardhini na kuviringika shaghala baghala, kila moja upande wake. Makomando wanagaragazwa vibaya na yale marobota makubwa, lakini kwa kuwa walikuwa mahiri kwenye kazi zao na kwa kuwa walishalifanyia mazoezi mara kadhaa tukio lile kabla ya siku ile, kila mmoja alifanikiwa kujirusha pembeni na kubaki akiwa amejilaza kimya kwenye majani mafupi ya eneo lile, macho yao yakitafuta uelekeo ambao kila mmoja aliamini kuwa ni kusini ya pale walipoangukia, wakiyaacha yale marobota makubwa kabisa yakiendelea kubingirika huku yakijizonga na yale maparashuti yaliyoyashusha.
Kule kwa wanakijiji wenye njaa, watalebani walikuwa wakiyafuatilia yale marobota kwa umakini kwa kadiri walivyoweza. Kwa namna fulani ambayo sio bahati mbaya, marubani waliokuwa wakiyadondosha yale marobota waliyaangusha mbali na ile mioto mikubwa iliyowashwa kuwaelekeza ni wapi yale marobota yaangushwe, na hii iliwapa nafasi makomando walioshuka na marobota yale kuweza kutumia kiza kilichopo, mbali na ile mioto, ili kijiweka mbali na marobota yale na kwenda kwenye jukumu lililokuwa mbele yao. Jukumu kubwa na la hatari sana…wenyewe waliliita ni jukumu la kujitoa muhanga…suicide mission. Kwa ajili ya mtu mmoja ambaye hata hivyo hawakuwa wakimjua kiukaribu wowote zaidi ya kuwa alikuwa akihitajika sana na nchi kubwa duniani, na kwamba malipo yao kwa kujitoa kwao kwenye kulitekeleza jukumu lile, yalikuwa ni makubwa sana kiasi cha kuhalalisha lolote ambalo wangekutana nalo ndani ya eneo lile lililoshindikana kabisa hata kwa mataifa makubwa yenye uwezo mkubwa wa kivita…
Kila mmoja alibaki akiwa amelala mahala pake, akitafuta ishara aliyoandaliwa kuitafuta mara baada ya kutua ndani ya eneo lile kusudiwa. Wakaiona. Kutokea kwenye kona moja ya eneo lile, hatua kadhaa kutoka kwenye moja ya marundo ya mioto iliyokuwa ikiwaka eneo lile, taa nyekundu ilikuwa ikiwashwa na kuzimwa kwa kufuata utaratibu maalum. Iliwaka mara nne kwa kuacha kiasi cha kama sekunde moja baina ya muwako mmoja na mwingine, kisha ikafuatiwa na miwako mingine mitatu ya haraka haraka. Ilikuwa ni mbinu maridhawa kwani kwa pale ile toch maalum yenye mwanga mwekundu ilipokuwa ikiwakia, haikuwa rahisi hata kwa mtalebani mwenye macho makali kiasi gani, kuweza kuutofautisha mwanga ule kutoka kwenye mwanga wa moto uliokuwa ukiwaka hatua chachekutokea pale.
“Mmeona?” Mmoja alisaili kwa mnong’ono mkali.
“Yah!” Mwingine alijibu, na wengine wawili nao walituma majibu yao kuwa wameiona ile ishara. Lakini hakuna aliyetoka pale alipokuwa amelalia tumbo, akiwa na silaha yake mgongoni.
Kule kwa wanakijiji, watalebani waliendelea kujificha huku wakiyatazama yale marobota yakiendelea kubiringika huku wakiwa wamewaamuru wanakijiji wote kutulia mahala walipokuwa. Marobota yalipotulia kila moja upande wake, bado watalebani waliojaa shuku na wasiyemuamini yeyote isipokuwa wao wenyewe, wanawazuia wanakijiji kuyasogelea. Wanayatazama kwa umakini mkubwa yale marobota kutokea kule walipokuwa, wakitaraji jambo baya kutokea. Lakini halitokei. Hatimaye wanatoa amri kwa wanakijiji kuyaendea yale marobota. Kelele za shangwe zasikika pale wanakijiji wanapokurupuka na kuyakimbilia marobota yale, na ndipo kule walipokuwa, wale makomando wanatambaa kwa kasi sana kuelekea kule ile ishara ilipotokea. Wakati watalebani wako makini kufuatilia harakati za wanakijiji kule kwenye yale marobota ya vyakula, hawatakuwa makini kufuatilia kitu kingine na hawataweza kuona wakati wale makomando wakitambaa kwa uficho namna ile kuelekea sehemu tofauti na kule yale marobota yalipokuwa.
Makomando wanafika pale ishara ilipotokea, na hapo wanakutana na mshirika wao, mwenyeji wao, raia wa Pakistani aitwaye Imraan Gopang. Naye akiwa amevaa nguo kama walizovaa wao, ila akiwa amebeba begi mgongoni na akiwa amening’iniza bunduki mbili mgongoni kwake, Imraan anawaongoza kwa usiri bila ya kuongea lolote hadi kwenye shimo la wastani mithili ya yale mashimo ya vyoo yatumikayo kwenye jamii nyingi.
Haraka haraka wanaufunua mfuniko mzito wa zege wa shimo lile, na tochi zilizounganishwa kwenye bunduki zao zinawaonesha ngazi za chuma zilizojengewa kwenye ukingo wa shimo lile, ambazo zingewateremsha hadi kwenye kichanja kikubwa cha chuma kizito ambacho kilikuwa kinakatisha kutoka upande mmoja wa mtaro mkubwa kabisa wa chini ya ardhi, hadi mwingine, na kuwa kama daraja la aina fulani..
Wale makomando wanne na yule mwenyeji wao wanaingia ndani ya shimo lile na kuufunika ule mfuniko wake kwa ndani. Wateremka hadi pale kwenye kile kichanja kirefu cha chuma kizito, sasa wakiwa ndani ya mtaro mkubwa wa chini ya ardhi. Kiasi cha kama mita tatu hivi chini ya daraja lile, maji machafu ya kitongoji kile cha Waziristan yalikuwa yakitiririka kuelekea kwenye mdomo mpana wa mtaro ule, ambao ulichomoza kutokea kwenye uso wa jabali refu sana, kiasi cha kama kilomita moja zaidi kutokea pale walipokuwa. Njia nyingi kutoka pande mbali mbali za nchi ile zilikuwa zikimimina vinyesi na majitaka kwenye mtaro ule mkubwa kabisa, ambao nao ulisafirisha shehena ile ya uchafu kwa hiyo kilometa moja zaidi kutokea pale wale makomando walipokuwa na hatimaye kwenda kuitiririsha kwenye mto mkubwa kabisa uliokuwa umbali wa mita zipatazo mia saba kwenda chini kutokea kwenye uso wa jabali refu ambalo juu yake ndipo kijiji kile cha Dargah Mandi kilikuwepo.
***Watu wakazi mtaroni! Lengo lao litatimia kweli? NJOO KESHO muda uleule...
Bora usiisome maana unacopy story nzima ili uandike Maneno hayo tuuKumbe ni hadithi za kutungwa napata tabu kusoma
Hutakaa uone hilo neno mkuu, maana mtunzi wa hadithi Hussein Tuwa ameacha kuiendeleza kwenye page yake ya facebook kwa sababu watu wanacopy na ku-share bila idhini yake. kwa hiyo ameamua kuandika kitabu..nasubiri nikiona neno end ndo nianze kuisoma. Plz siku ikiisha mniite
shukrani mkuu kwa maelezo murua maana ningeisoma ningejitia genye tu halafu nisingefika kileleni hataHutakaa uone hilo neno mkuu, maana mtunzi wa hadithi Hussein Tuwa ameacha kuiendeleza kwenye page yake ya facebook kwa sababu watu wanacopy na ku-share bila idhini yake. kwa hiyo ameamua kuandika kitabu..
sisi wenyewe tuko kwenye foleni ya kusubiri hicho kitabu
Alafu ni kali balaa, huyu jamaa ni Messi wa utunzi wa hadithishukrani mkuu kwa maelezo murua maana ningeisoma ningejitia genye tu halafu nisingefika kileleni hata
Acha ku quet hadithi kwa ujinga unao fanyaKumbe ni hadithi za kutungwa napata tabu kusoma