Wimbo wa Ali Kiba umetumika kuandika Hukumu Mahakamani

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
5,351
7,635
Sisi Wanasheria tuna dhana moja isemayo, "writing a judgment in an art". Yaani uandishi wa hukumu ni sanaa.

Majaji wengi hasa wa zamani walikuwa wanaandika hukumu nzuri sana ambazo zinakuwa na vionjo mbalimbali vinavyomfanya msomaji (hata kama siyo mwanasheria), avutiwe kuisoma.

Kwenye kesi ya Jamhuri Vs Frederick Michael John @ Bashite iliyosikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Musoma katika kesi ya jinai na. 84 ya mwaka 2022, ambapo Frederick anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Dorice Samson Okech na mdogo wake Dorice aitwaye Nickson Charles Sendama, Jaji Mahimbali, katika ukurasa wa 2 wa hukumu yake ameandika yafutayo, nanukuu kwa Kiswahili (ingawa hukumu imeandikwa kwa Kingereza);

"Kesi hii inahusisha wapenzi (ambao hawakufunga ndoa) waliogombana na kusababisha mapenzi yao kufikia ukomo, hali iliyosababisha kifo cha mwanamke na mdogo wake ambaye hakuwa na hatia. Nalifananisha tukio hili na maudhui ya mashairi ya mtunzi na mwanamuziki Ali Kiba @ King Kiba kwenye wimbo wake "Mahaba" ambao una shairi lifuatalo..

Siku hizi hakuna mahaba, yeah mahaba...

Ni neema ukiwa unahema...

Nafsi yangu inasema bora nimpende tu alonizaa...".

Hukumu ikaendelea kwa Mh Jaji kuuchambua ushahidi na mwisho wa siku mtuhumiwa (Frederick) akahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Nadhani wakati mtuhumiwa anasomewa hukumu alijua anaachiwa aliposikia Jaji anaunukuu wimbo wa Ali Kiba, kumbe balaa lilikuwa linafuata.

Hongera sana Ali Kiba. Team Simba mpo?
 
Huyo Hakimu asijipendekeze, Ali Kiba apendi show off.
 
Sawa Dogoo!!Naona na wewe umeamua kujipakulia minyama!!hutaki cheza mbali kabisaa yaanii!!
 
Back
Top Bottom