Wezi wawili wakiungua moto mbagala kwa Mangaya - Tutaendelea kujichukulia sheria mkononi hadi lini

Roho za watu alizoziuumba mwenyez Mungu haziendi hivi hivi kwa mali alizozitengeza Mwanadamu, hakika hao walio wachoma hao binadam Mungu anajua atavyowalipa!!
 
10292142_626801474079125_8675300846181144242_n.jpg

Wezi wawili wakiungua moto mbagala kwa mangaya


Siwezi kuamini kama:
  • Viongozi wa serikali za mitaa
  • Wapenda Mungu
  • Wenye utu
  • Wanaoheshimu haki za binadamu
  • wenye kujali usilotaka kutendewa usimtendee mwingine nk
Wanaweza kujichukulia sheria mkononi bila huruma. Pengine walichokiiba hawa vibaka wawili ni pipi huku adhabu ni kuondoa uhai wao bila huruma na hadharani wakishuhudiwa na waliowasulubu.
wewe hujawahi kuibiwa,au unaundugu na hao vibaka,kweli ktk dunia ya Leo unaleta hoja za kumtetea kibaka?
w
 
Hakuna asiyewahi kuibiwa maishani, kangu nikiibiwa najua nivyoibiwa nitakavyoweza kupata vingine, lakini hii ya kwa macho yangu nishuhudia kutoa roho ya mto, na kabisa watoto wadogo wanashuhudia hilo ni malei gani kwa jamii? Sikubaliana kabisa na huwezi kunibadili katika hili, ni dhambi kusitisha uhai ambao ni zawadi ya kila mmoja wetu toka Kwa Muumba.

Mwizi ni muuwaji akikuwahi anakuua,na wewe ukimuwahi toa roho kabisa huyo shetani.
 
Ni wapi kulikoandikwa kwamba mshahara Wa dhambi ni neema? Hebu tusijifanye vipofu wa akili!! Juzi tu tumesikia wamevamia kituo na kuua askari polisi! Hawa jamaa wakija kwako ni ama zako ama zao, sasa kwa nini sisi tuwahurumie? Wachomwe tu!


Usifananishe vibaka na Majambazi!! kwa majambazi kwanza mwananchi wa kawaida kumdaka ni shughuli ila walamba unga wepesi tu..
 
Mwizi ni muuwaji akikuwahi anakuua,na wewe ukimuwahi toa roho kabisa huyo shetani.

Kila auwae kwa upanga...atakufa kwa upanga...wee endelea kuhukumu mwenzio iko siku mungu atakulipa..ogopa sana damu ya mtu ina nguvu
 
Ni kama mtu anakukera unamtukana....hawa wananchi wamechoka wakaamua kuua na kuchoma. Mungu anaweza kueleza dhamira zao lakini sisi wanadamu hatuwezi maana machungu yako huenda yakawa kicheko cha mwenziyo na uchungu wa wana kwa Mangaya huenda ukiusikia utadhani ni utani....God is the judge na mara nyingine anaruhusu hilo litendeke kwa makusudi ya kufundisha ama kuonya wala usiogope God is still incharge...yetu ni kujifunza
 
Kiukweli kuibiwa kunauma na kunarudisha sana nyuma maendeleo ya mtu lakini suala la kuchukua sheria mkononi kiasi cha kuwachoma moto hao wezi sio cha kiungwana.Unafikiri watoto wadogo tunawajengea mawazo gani na fikra gani.Jamani tuwaadhibu sana lakini isifikie kuwauwa.
 
Umenena kwa busara kubwa sana mkuu.

Dah! Najau hao jamaa wana wazazi hususani Mama, mara nyingi ukikuta mzazi wa kike anavyomlilia mtoto wake alie uwawa kinyama hivyo kisa kakwapua kitu hulia kwa machungu sana!! Japo wizi sio mzuri!!!
 
Wanakera sana hao vibaka, ni watu wanaorudisha maendeleo ya watu nyuma.Wakati wengine wanapambana na maisha kwa kazi ngumu wao wanawaza kukwapua na kukimbia.Angalia kikundi kama cha mbwa Mwitu na vibaka wengine jinsi wanavyotusumbua mitaani.
Acha wapewe funzo hayo ndo maisha waliyochagua na huo ndo mwisho wao na wao wanalijua hilo.
 
hawa vibaka nao wamezidi wanapenda pesa za haraka ndo matokeo yake wewe unayejifanya unawaonea huruma kwa nini hujawaokoa umekimbilia kuwek a picha humu mnafiki mkubwa wewe
 
God is the judge na mara nyingine anaruhusu hilo litendeke kwa makusudi ya kufundisha ama kuonya wala usiogope God is still incharge...yetu ni kujifunza
Habari za mungu zinaingia vipi hapa kuwachoma vibaka moto ni mungu, mungu huyo kama asingetaka wawe vibaka basi si angewashushia neema zake za kuweza kumudu maisha. Unless labda una imply mungu katuumba na katuwekea mazingira ya upendeleo hivyo kuwa kibaka ni gods fate, that includes the dangers that come with it including being burned alive.

Sina tatizo na jambazi la bastola kuchomwa kwa sasa, lakini mwizi wakawaida tu ambae kanyofoa sijui cheni ama kapanda ukuta kuanua nguo uani kwa mtu; kwakeli swala la kuchomwa moto ni punishment iliyopitiliza.

Hawa ma-judge, maloya, mapolisi, na taasisi zote zinazojishirikisha na mambo ya uhalifu as in rehabilitation centers or reducing crime ni wasomi wa maswala ya uhalifu, unajua wazi sababu za mwizi wa wakawaida kama sio madhara ya madawa ni poverty fueled act. Kwanini huyo mtu umchome moto kutokana na mazingira yake na kwanini serikari ambayo inashindwa kuja na sera za kuwasaidia vijana in the first ishindwe kukemea hawa watu kupewa adhabu ambayo sio stahiki kwa dunia ya leo.

Waafrika tusipo jirekebisha na kuanza kudai siasa za maendeleo bila ya ushabiki tutabaki maskini wa muda mrefu sana. Yaani muda unaotumiwa kutukanana majukwaani na wanasiasa na sisi kuvalia ngojera ni ishara ya kuwa hatuko tayari kudai vile vinavyotugusa sio sisi na jamii inayotuzunguka, mtoto wa shangazi akikosa kazi anaweza kuwa gharama kwako na kama wewe huwezi option nyengine ni hii.

Huwa najiuliza sana wale watoto wa mtaani wanao lala ovyo wanaishiaga kuwa maisha gani huko mbele wengi wao. Ukute ndio hawa tunaowachoma moto kila kukicha, kisa kadakua nguo uani this is immoral.
 
Hivi kifo ni adhabu au wajibu wa kila mmoja wetu kwenye maisha? dawa yao ilikuwa kukata mikono tu ambapo tuone kama wataiba kwa kutumia miguu..

Ukishawakata mikono,mzigo wa kumtunza huyo kibaka anapewa nani?
 
kuibiwa jamani kunarudisha maendeleo nyuma
ni vyema kujichukulia sheria mkononi kwani hao wezi wamezidi
ukiwapeleka kuleeee chumba cha jirani inakuwa........
 
Kama Waziri Mkuu Mwwenyewe anatamka Polisi wawapige Raia na anashinda Kesi Mahakamani unategemea nini kwa Raia wakimshika Kibaka.
 
Kama hawa watu wanachukia wezi kiasi cha kuwaua na kuwachoma moto. Wangefanya haya kwa wanaoingiza unga,mafisadi,wanaoua tembo.Hawa vibaka yawezekana ni matokeo ya ugawananyi mbaya ya keki ya taifa.Kiukweli ni vibaya kujichukulia sheria mkononi
 
Back
Top Bottom