Wezi na Wizi wa Magari umerudi kwa kasi ya 5G ni wapi tunakosea?

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,924
4,481
Ndani ya week 2 kuna gari tano (5) Zimeibwa Tabata, Gari Mbili zimeibwa Mlimani City. Moja ya Tabata imeibwa karibu kabisa na kituo cha Polisi. Mlimani City jamaa yangu kaibiwa Toyota Crown. Naambiwa pia Kimara kuna gari mbili zimeibwa moja ikiwa imepark nje Bar na nyingine Ndani.

Naanza kujiuliza ni wapi tumekosea? je wahusika wa huu wIzi wamerudi toka likizo? au wamepata kibali wapi cha kuendesha shughuli hizi bila woga wala kificho? nadhani huu ni mpango wa watu fulani kuchafua Serikali ionekane haifanyi kazi pamoja na Jeshi letu la Polisi.

Kuna maneno mengi yakiwemo kuwa wahusika wa Wizi huu ni pamoja na Polisi wenyewe, Mtandao wenye watu wakubwa au watoto wa wakubwa na watu maarufu ambao waliamua kipindi flani kupumzika sasa wame toka mapumzikoni na kurudi kazini. kilio kimekuwa kikubwa sana kwa wananchi wa kipato cha chini ambao ndiyo wamekuwa waathirika wakubwa wa mambo haya sababu gari zao ndizo huibwa sana kuliko ma Vieti n.k

Serikali nini shida ?tunategemea kuwa ninyi ndo mtusaidie kupitia kodi zetu ambazo tunazitoa ili muajiri watu ambao watatupa amani tunapofanya shughuli zetu nyingine. then kwa nini tunyanyasike hivi utadhani tunaishi Colombia au Mexico miaka hiyo? Tunaomba Mh, Rais, Waziri na Wakuu wa Usalama mliangalie jambo hili maana tunakoelekea nchi hii itakuwa sasa ni kama watu wameamua kuishi watakavyo. amani na utulivu vitafutika.

Najiuliza ni wapi tunakosea? yaani kwa sasa ukiwa na gari lako roho inakuwa juu juu tu ukiwa ofisini kila wakati unachungulia nje kuona kama gari ipo au wamechukua.ukilala hulali muda wote ni kuangalia kama gari ipo au wamechukua mwishowe hata hatuwezi fanya tendo la ndoa unakuwa juu juu tu hisia zitatoka wapi ukiwaza usalama mdogo?

Unakamua issue unakimbia nje kuangalia kama gari ipo ukirudi unakuta mashine imeshalala na mwenzi wako analalamika ulimwacha akiwa anataka kumaliza... hali hii mpaka lini? kazi hazifanyiki kwa amani sababu muda wote tunawaza hiki kigari changu kipo kweli au watu wametambaa nacho?
 
Dawa ni kufungia king'amuzi uweze kui-track... Ule msemo wa chunga mzigo wako usiishie kwa abiria tu uwe applied na kwa wenye magari, na sasa iwe dereva chunga gari yako!
 
Unailalamikia serikali kuwa wazi tuu kwamba serikali sasa ya wezi tujue siyo kupindishapindisha maneno.
 
Mdau anasema kwa sasa hata usiku hapigi show vizuri....πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…