Wewe ni mfugaji? Uliza swali lolote la kitaalam nikusaidie

[QUOTE="Mshawa, post:
46cf80e7b416f1f90b05d888f36133df.jpg
 
Aikaruwa Hawa Broiler wapo wa jinsia zote ila wakiwa wadogo ni vigumu kuwatofautisha, kadiri wanavyokua ndio utaweza watofautisha.

Kwa kuwa hufugwa kwa muda mfupi wiki 4 hadi 6 na matumizi yao ni kwa ajili ya nyama ndio maana huchanganywa pamoja (tetea na jogoo) na kufugwa pamoja.

Ila kwa upande wa kuku wa mayai (layer's) tetea na jogoo hutengwa tangu wakiwa vifaranga na tetea huuzwa bei yake na jogoo hutupwa au hutolewa kwa bei ndogo sana maana ni garama kumfuga na ukuaji wake ni wa pole pole, na Kwa kuwa hana faida nyingine zaidi ya kupata nyama yake labda na mbegu yake.

mkuu unisaidie kitu kimoja kuku wa mayai(layers) inatakiwa uwape chakula kwa kipimo kipindi wanaanza kutaga mpaka watakapomaliza sasa hiyo resheni mfano ya kuku 10 wanasema ni kilo 13 kwa siku sasa chakula hicho unakiweka asubuhi chote au unaweka kilo 6.5 asubuhi then jioni unamalizia 6.5.... msaada tafadhali.... na hvi sababu za hawa kuku wa mayai kutaga mayai madogo ni nini.....(ni aina ya mbegu au chakula)
much respect
 
Huuhitaj dagaa wakulisha KUKU wako, kama unahtaji nipe oda niko mwanz,KWA mawasiliano 0685427278
 
mkuu unisaidie kitu kimoja kuku wa mayai(layers) inatakiwa uwape chakula kwa kipimo kipindi wanaanza kutaga mpaka watakapomaliza sasa hiyo resheni mfano ya kuku 10 wanasema ni kilo 13 kwa siku sasa chakula hicho unakiweka asubuhi chote au unaweka kilo 6.5 asubuhi then jioni unamalizia 6.5.... msaada tafadhali.... na hvi sababu za hawa kuku wa mayai kutaga mayai madogo ni nini.....(ni aina ya mbegu au chakula)
much respect
Ukiwapa chote kg 13 asubuhi watakifakamia na mchana kutwa watakua wamekimaliza na kuanza kudonoa vyombo vya chakula, hivyo ni vyema ukakigawa 6.5 asubuhi na kingine unamalizia jioni saa 10

Kuku kutaga Mayai madogo hutokea mwanzoni waanzapo kutaga kwa kuwa ile njia ya uzazi bado ni ndogo na kadiri anavyozidi kutaga inaongezeka na size ya yai pia inaongezeka lakini pia lishe ikiwa duni au ikizidi yaweza jaza mafuta na kupelekea kutaga Mayai madogo

Pia mazingira ya kufugia yakiwa ya joto kali , kukosa mwanga wa kutosha na hewa yaweza pelekea kutaga Mayai madogo (kiumbo) na uchache
 
nina mpango wa kuanza ufugaji wa nguruwe sasa nashindwa kupata namna ya kujenga mabanda kwa ajili ya hao nguruwe, naomba ushauri wa jinsi ya kujenga mabanda ya kisasa coz nataka nitumie tofali na sio mabanzi, pia nataka kufahamu vipimo kwa kila chumba na idadi ya nguruwe kwa kila chumba kiutaalamu zaidi. Asante
 
Tangu nimeanza kufuga kuku wa asili kwa nia ya kuniongezea kipato nimegundua kuna ugonjwa unaitwa coccidiosis. Huu ugonjwa umenikumbusha ule msemo avumae baharini papa... Huu ugonjwa ni hatari sana kuliko yale magonjwa yanayotajwa sana! Naomba kufahamishwa unavyoenea, unavyotibiwa na unavyokingwa.
 
huu ugonjwa ni ugonjwa ambao usababishwa na bacteria aina tofauti za spp ya eimeria, niugonjwa ambao hata binadamu uupata pia

ugonjwa huu uenea kutoka kwa mnyama mmoja kwenda mwingine kwanjia ya myama kula chakula au maji ambayo yanakua na bacteria hao

dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kuhala damu au kinyesi chenye kuchanganikana na damu hii nidalili moja kuu ikifuatiwa na mnyama kua dhaifu kupungua uzito n.k

huu ugonjwa unatibika kwa dawa aina ya amprolium au nyingine zilizo na salfa ndani yake

njia yakucontrol huu ugonjwa ni usafi wa banda na vyombo anavyotumia kulia na kunywea maji mnyama
 
Asante sana mdau
 
Je ngombe wa kienyeji anatoa maziwa kiasi gani kwa siku? na kwa msimu? na je unaushari gani wa ngombe hasa wanaovumilia mgonjwa kama hao wa kienyeji? watoa maziwa ya kutosha na wawe na uzito mzuri kwa ajili ya nyama?
 
Kwa uzoefu wangu kila kiumbe kina mazoea yake na kikisha zoea kuishi namna fulani ukija kukibadilishia life style shida hujitokeza. Ng'ombe wa kisasa pure kama utaanza kumzoesha maisha ya kawaida yaani yakwenda machungani asubuhi na kurudi jioni atazoe na maisha yatakwenda vizuri. Ila usije ujanunua ng'ombe aliezeekea kwenye zero grazing alafu ukaenda kumchunga hachukui muda utaangua kilio.
 
Niko poa unalenga kufuga nguruwe kwa minajili ipi ..... Kunenepesha au kuzalisha nikimaanisha kuzalisha watoto na kuuza au ni kibiashara tu...

Ikiwa ni kibiashara set hall mojo lenye partition 3 ambapo utalelea watoto toka wanapoacha kunyonyo kwa marika (umri) tofauti kisha tengeneza vyumba ya sq meter 3*4 ambapo utakuzia vijana wa nguruwe 3~4 kwa kila chumba hadi kufikia umri wa miezi 7 ambapo utaamua uwachinje ama uwazalishe

Pia tenga vyumba vya idadi utakayo kulingana na nguruwe wako vya ukubwa wa sq meter 2 kwa 3 kwa ajili wazazi ambao hapa kila mzazi atakaa peke yake na kunyonyesha watoto kwa muda wa wiki 7 hadi 8 kabla hujamwachanisha na watoto

Pia tenga chumba cha wamama waliotenganishwa na watoto kila mmoja atahitaji sq meter 5 kwa ajili ya kula na kupumzika kwa muda wa siku 25 hadi 30 kabla hajarudishwa tena kwa duke

Pia tenga chumba cha dume ambapo utamweka dume bora la mbegu na kisha kumpelekea majike yaliyotayari kuzalishwa kiwe na angalao sq meter 6 kwa 5, kiwe na bwawa la kuogelea, pia kiwe na sehemu kubwa na za kutosha za chakula na Maji kiwe na milango na kuta imara

Nimejaribu kuandika kwa uzoefu nilionao na pia kwa kuwa hujasema idadi ya nguruwe unaotaka kufuga.
 
Nataka kufuga nguruwe ila sijui chochote kuhusu nguruwe na jike la uhakika linapatikanaje. Asante
 
Afadhali,aiseee nafuga kuku wa kienyeji ila vifaranga wangu wanakufa sana na ndui,na wanaobaki sometimes inabidi kuwalisha kwa kuwalazimisha kama watoto jna kuwalazimisha dawa hasa alovera orijinal ile wengine wanasurvive wengine wanakufa,then wengine wananyonyoka manyoya na wanadonoana sana tatizo n nini mkuu
 
Habari za saa hizi waungwana naomba kuuliza ni sehemu gani wanauza parent stock nataka niwe natotolesha mi mwenyewe
Nipo Arusha
 
Habari,nafuga Kuku wa asili naomba msaada kwani nimegundua vifaranga vya kuku wanatoa kinyesi cha njano ila hakijaganda kwenye manyoya pia wamechangamka. Je hii inaashiria nini??
 
Niko poa unalenga kufuga nguruwe kwa minajili ipi ..... Kunenepesha au kuzalisha nikimaanisha kuzalisha watoto na kuuza au ni kibiashara tu...

Ikiwa ni kibiashara set hall mojo lenye partition 3 ambapo utalelea watoto toka wanapoacha kunyonyo kwa marika (umri) tofauti kisha tengeneza vyumba ya sq meter 3*4 ambapo utakuzia vijana wa nguruwe 3~4 kwa kila chumba hadi kufikia umri wa miezi 7 ambapo utaamua uwachinje ama uwazalishe

Pia tenga vyumba vya idadi utakayo kulingana na nguruwe wako vya ukubwa wa sq meter 2 kwa 3 kwa ajili wazazi ambao hapa kila mzazi atakaa peke yake na kunyonyesha watoto kwa muda wa wiki 7 hadi 8 kabla hujamwachanisha na watoto

Pia tenga chumba cha wamama waliotenganishwa na watoto kila mmoja atahitaji sq meter 5 kwa ajili ya kula na kupumzika kwa muda wa siku 25 hadi 30 kabla hajarudishwa tena kwa duke

Pia tenga chumba cha dume ambapo utamweka dume bora la mbegu na kisha kumpelekea majike yaliyotayari kuzalishwa kiwe na angalao sq meter 6 kwa 5, kiwe na bwawa la kuogelea, pia kiwe na sehemu kubwa na za kutosha za chakula na Maji kiwe na milango na kuta imara

Nimejaribu kuandika kwa uzoefu nilionao na pia kwa kuwa hujasema idadi ya nguruwe unaotaka kufuga.

Duh mkuu Shawa kumbe huyu jamaa naye anahitaji Swimming Pool? Sikuwa nafahamu hili.
 
Back
Top Bottom