Wenye uzoefu na maisha ya ndoa please nishaurini, muhimu sana

So basically, unatuambia kuwa mapenzi yenu yana thamani isiyozidi 2m? Ok. Hiyo 2m ni return ticket, ama? Sema anatoka wapi watu wakupe options.
 
Mtoa mada ni mvulana sio mwanaume, just ignore him, hivi mkeo unawaza kuja kwake against biashara! hujitambui au hujielewi? Fanya biashara kwanza nae afanye yake kule afu utakuja tena hapa ukilialia kama zuzu. Umenikera sana kwa kukosa akili
 
Kaka mke hujiulizi hivyo mbona, kwanza kumlinganisha na biashara yamaanisha hauko tayari aje na huitaki familia.

Mi nadhani swali la ww kuuliza ni atafikaje huku kwa bei rahisi (ikibidi magendo) na sio kuja au asije.

Kuhusu ugumu wa maisha sijui kumlisha na nini, ulipooa ulitegemea ale polisi? Kimbia shida na sio majukumu.
 
Ok, ushauri utapata. Lakini jibu swali hili, umesema wife which means legitimately married. (Yes/No)? Kama ni yes, anatoka nchi gani? Kama ni No huhitaji ushauri wowote maani huyo si mkeo it's some kind of illusions on your head.
 
Hakuna mapenzi hapo....wewe unapigia hesabu nauli ya yeye kuja..naye anakwambia umtumie nauli ndio akuje.

Kuna jamaa alifanya mpango wa siri kumtoroka mke wake...akiwa kwenye ndege wanakaribia kutua wanakokwenda aligeuka nyuma hakuamini macho yake kumuona mkewe yupo siti kadhaa nyuma yake.....walipotua akamuuliza mke wake "kwa nini umefanya hivi na umepata wapi nauli"...mke akamjibu kwa swali "wewe kwa nini umefanya hivi na mimi ni mkeo au ni nani kwako?"

Ni kwamba jamaa alipata kazi ya muda mfupi na ya malipo makubwa nchi nyingine na moja ya masharti aliyopewa ni kwenda peke yake bila mkewe....na ili isiwe tabu aliamua kumtoroka mke ili baadae ndio ampigie simu ampige fiksi coz aliamini kuwa ni rahisi kuomba msamaha kuliko kuomba ruhusa.

Sasa huyo anayesubiri nauli jiulize mara mbili.
 
Hey guys NAOMBENI USHAURI WENU, Najua ushauri wa wengi huwa waleta uelewa na akili ya kuambiwa changanya na yako ili vitu viende sawa, mimi na mke wangu tumekuwa mbali kwa muda wa karibu miaka miwili sasa kwa kuwa yeye ni mtu wa nchi nyingine nami ni mtanzania na to be honest i really miss my wife, The thing huko aliko hana pesa wala Biashara nami hapa nilipo Bagamoyo nina vijibiashara vyangu vinavyonipa just mlo wa kila siku, However hivi juzi mke wangu ameniambia nimkatie ticket ya ndege ili aje Tanzania ambapo nimepiga mahesabu itani cost almost 2million, nimefikilia hiyo pesa si ni bora niwekeze kwenye kuongeza mtaji wa biashara na nikifanikiwa zaidi ndo nimtumie, au kama ungekuwa wewe ungefanyaje, kumtumia nauli na akija kila kitu kinakuwa juu yako kuanzia kula kwake hadi kulala as yeye hatokuwa na kazi AU umuache na hiyo pesa uongezee mtaji wa biashara hadi utakapo kuwa kibiashara ndipo umlete???? Naomba mawazo na maoni yako.


= nimefikiria
. Na hapo kwenye heading mwombe Mhariri arekebishe.

Nishaulini = nishaurini

Halafu kwenye mitandao ya kijamii ambamo wanaingia watu wa jinsi na umri tofauti si vyema kuanza na "hey guys" kwani wengi siyo "guys" na si heshima nzuri.
 
1. huyo ni mke ambae mmefunga ndoa kabisa?
2. kinachowafanya msiishe pamoja ni nini?
 
kama hali yako unauwezo wa kumtumia nauli ni bora umtumie alafu akishafika mtabangaiza hivyo hivyo
 
Ok, ushauri utapata. Lakini jibu swali hili, umesema wife which means legitimately married. (Yes/No)? Kama ni yes, anatoka nchi gani? Kama ni No huhitaji ushauri wowote maani huyo si mkeo it's some kind of illusions on your head.

Yes,she is my wife and is coming from Thailand.
 
Back
Top Bottom