Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 365
MDAU ANAOMBA USHAURI
"Mimi ni mtoto wa tatu kuzaliwa kwenye familia ya watoto wanne kwa wazazi wetu huko Moshi - Kilimanjaro.
Nilikuja mjini Dar es Salaam kwa kusaidiwa na kaka zangu wawili hasa huyu wa pili kuzaliwa.
Kwa taratibu za kule kwetu uchagani huwa tuna desturi ya kushikana mkono yaani kusaidia wengine pale unapofanikiwa.
Kaka mkubwa alikuwa wakwanza kufanikiwa nae akamleta mjini kaka yangu wapili kuzaliwa ambaye naye baada ya kufanikiwa akanileta mimi mjini.
Ni kweli katika kupambana kwangu na support niliyopewa nilifanikiwa kumuliki biashara kubwa mjini na nyumba nzuri ya kuishi. Kiufupi maisha yakawa mazuri kimtindo.
Mdogo wetu wa mwisho alipomaliza kidato cha nne kaka zangu wakaniambia nimchukue dogo aje mjini nae nimfundishe maisha kama nilivyosaidiwa mimi.
Hilo halikuwa tabu kwangu nami nilifanya hivyo na dogo akaja mjini akawa anaishi kwangu. Nikamwingiza kwenye biashara zangu kwa lengo nae apate uzoefu ili hata siku nikimfungulia biashara yake basi awe anajua kwa kuanzia.
Nikikaa nae kwangu kwa miaka miwili. Kuna siku alikuja kuniambia kuwa kwasasa amekuwa na anao uzoefu mzuri hata wa kujitegemea mweyewe akaomba nimsaidie pesa ya mtaji akaanze kufanya biashara zake nami sikuwa na hiana nikafanya hivyo.
Nilimuuliza anataka kufanya biashara gani, akaniambia anataka kufanya biashara ya kuuza nguo za kiume. Nilimwambia atafute flemu kisha nilimkabidhi milioni kumi ya kuanzia biashara na baada ya miezi minne nilimpa tena milioni tano kwahiyo jumla ikawa milioni 15.
Hivyo akaondoka nyumbani na kwenda kuanza maisha yake.
Lakini nilimwambia anipeleke nikaone dukani kwake ili nikaangalie pia na mwenendo wa biashara ananizungusha tu mala kesho keshokutwa siku zinazidi kwenda.
Baada ya miezi kama saba hivi au nane akanifuata kazini kwangu anaomba nimsaidie tena milioni tano mambo yake hayaendi vizuri. Kwakuwa najua biashara sometimes zina changamoto nilimpa kama kawaida.
Kuna mtu alikuja kuniambia ndugu yangu mbona unapoteza sana pesa kwa huyo mdogo wako bila mpangilio!! Kumbe siku zote hizo mimi nampa pesa lakini hakuna biashara yoyote anayoifanya. Yaani pesa zote anaenda kufanyia starehe na mademu wa Dar es Salaam, kila kiwanja cha starehe anakijua yeye.
Nilikuja kumwambia tena anipeleke kwenye biashara aliyodai kuwa amefungua ikawa ugomvi mzito eti anasema yeye sio mtoto mdogo hivyo tabia za kumfuatilia fuatilia nikome kabisa hasije kunifanyia kitu kibaya ambacho sitakuja kusahau maishani mwagu.
Baada ya tukio hili niliwafata kaka zetu hao wawili na kuwaambia kuwa kwasasa dogo akikwama tena kimaisha sitamsaidia kwasababu nimeshamsaidia sana lakini hasaidiki na kunitolea kauli chafu.
Hapo tuliitwa kikao hadi wazazi kutoka kwetu kijijini huko Moshi walikuja. Dogo analalamika kuwa hata kwangu nilikuwa namnyanyasa sana ila mke wangu tu eti ndio alikuwa anamuonea huruma mala mojamoja ila mimi eti nina roho mabaya sana ya choyo na chuki dhidi yake.
Dah! Niliumia sana. Nilishikwa na hasira hadi nikashindwa kuongea chochote. Kwa jinsi dogo alivyokuwa anaongea kwa sauti ya juu kaka zangu na wazazi wetu wote walimuamini na kuwa upande wake.
Basi ili kuondoa lawama ilibidi nikope pesa benki na kuweka nyumba yangu kama dhamana. Pesa ile niliyokopa nikampa tena yeye lakini kwa makubaliano kwamba tutasaidiana kulipa deni hilo nae akakubali japo kwasababu tulipeana kifamilia hatukua na maandishi yoyote.
Baada ya rejesho la kwanza dogo aliingia mitini. Nikipiga simu hapokei, kuna siku alipokea aliniambia nisimtafute tena nijue maisha yangu hata akifa nisimzike na nikifa hatokuja kunizika. Kwakweli kama kaka niliumia sana, mimi sijaona sababu ya kwanini tufikie huko.
Hivi ninavyokwambia ule mkopo nilishindwa kurejesha wote peke yangu na biashara zangu ziliyumba sana na kufirisika kabisa. Hivyo, benki ile walichukua nyumba niliyoweka kama dhamana na kuiuza. Nimebaki sina pa kwenda na sina wa kunishika mkono.
Mtihani nilionao ni mkubwa mmno. Nilianza maisha upya na kwenda kupanga chumba cha bei nafuu huku Mbagala. Kutokana na ugumu wa maisha, mke wangu nae amenikimbia na kuniachia watoto wawili wadogo. Mmoja ana miaka 6 na mwingine ndio kwanza ana miaka miwili na nusu.
Kwa taarifa nilizozipata, mdogo wangu kwasasa maisha yake yamemwendea vizuri.
Lakini kinachoniumiza zaidi hadi nahisi kuchanganyikiwa, mdogo wangu kamchukua mke wangu anaishi nae kama mume na mke na teyari mke wangu ana ujauzito wake.
Dah!! Nikisema sana nitaishia kumkufuru Mungu, acha nisubiri ushauri wako.
Je, kuna hatua zozote za kisheria ninazoweza kuzichukua dhidi ya mdogo wangu juu ya haya yote yaliyotokea?"
MWISHO WA KUNUKUU.
@ Emmanuel Ngowi
-Mbagala Dar es Salaam
Posted By : Mr George Francis.
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com