Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
"Nendeni mkamdai Kikwete"
Hii ni kauli ambayo msanii Wema Sepetu ameitoa na kwa kweli imeusononesha sana moyo wangu. Sii kauli ya kiungwana kujibiwa watu wale waliomsaidia Rais Magufuli kuingia ikulu. Ole kwa yule aliyetoa majibu hayo!
Nadhani kauli hii itaweza kuusononesha sana moyo wa rais mstaafu ndugu Jakaya Kikwete ambaye alifanya kila liwezekanalo "liwe la kifedhuli au la haki" kuhakikisha Magufuli anashinda hasa kutokana na ule ushindani mkali uliokuwepo.
Ni kauli inayoendeleza udhihirisho wa kiburi na ulevi wa madaraka vilivyoujaa utawala huu wa awamu ya tano! Si kauli nzuri hata kidogo.
Majibu ya hovyo yanayotolewa na baadhi ya watendaji kwenye huu utawala kama haya yanadhihirisha kuwa watanzania bado tunajithibitishia wenyewe jinsi tulivyopotea njia.
Aidha kusukumiwa mzigo huu wa wadai wa CCM kwa Kikwete kunaendelea kudhihirisha utu wake na uungwana ambao mimi ni miongoni mwa wadau tunaolia machozi makuu kuukosa na kujikuta tukitumbukia tusikokujua. Kwa haya siamini kama mdai mwingine Shigongo yu salama na ahadi aliyopewa hivi karibuni.
chadema chadema chadema Wemas pawa!