Wema Sepetu akutwa na hatia ya kukutwa na Madawa ya kulevya! Alipa faini na kuachiwa huru

Sir Lindege

Member
Sep 10, 2013
35
181
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Ijumaa, Julai 20, 2018 inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu na wenzake wawili.

Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu tayari amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili.

Hukumu ya kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Mrembo na mwigizaji Wema Sepetu imeanza kusomwa na Hakimu Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam muda huu.

=======

IMG_20180720_122719.jpg

Msanii wa filamu ambae pia alikuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu amekutwa na hatia ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya.

Ahukumiwa jela mwaka mmoja au kulipa faini ya milioni 2.

Washtakiwa wawili kwenye kesi hiyo ambao ni wafanyakazi wake wa ndani wameachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia

Habari zaidi, soma=>Sakata la Madawa ya Kulevya: Wema Sepetu afikishwa Mahakamani, apata dhamana

Mkemia Mkuu: Mkojo wa Wema Sepetu ulikuwa na bangi


Wema amelipa faini, wakili wake, Msando amezungumza



=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
Back
Top Bottom