screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,829
- 15,791
Nianze kwa kuwapongeza WCB kwa hatua waliyofikia kuisimamisha lebo na kuwa lebo bora zaidi Afrika Mashariki, na moja ya lebo bora Afrika.
Niwapongeze kwa kuweza kuviinua vipaji ambavyo vilikuwa havitambuliki kabisa kwenye ulimwengu wa muziki na kuweza kupokelewa vyema, vipaji hivyo ni Harmonize na Rayvanny.
Niwapongeze tena kwa kufanikiwa kumuibua tena msanii mwenye kipaji cha hali ya juu Rich Mavoko ambaye alikuwa anaelekea 'shimoni' na anaendelea kufanya vizuri na kupata riziki kupitia muziki, pengine bila WCB tungekuwa tunamsikia kwenye stori za ngada kama ilivyokuwa kwa Ray C alipokuwa Kenya, Queen Darlin nisimzungumzie maana nahisi kaingia pale kama dada wa bosi, si kipaji.
Baada ya pongezi nije kwenye hizi new signings ambazo ni Lavalava na Maromboso, nikianza na Lavalava nilijaribu kuwa mvumilivu nisimjaji mapema niendelee kumsikiliza ila pamoja na kumpa muda na kusikiliza nyimbo zake zaidi ya 4 sijaona kama ana impact kubwa, nyimbo zake ni nzuri ila ni za kawaida sana, hazistui yaani.
Unajua msanii anapokuwa kwenye lebo kubwa tunatarajia makubwa sana sasa unapotoa nyimbo za kawaida lazima tushangae umeaminikaje kuwa pale, pia nikija upande wa Maromboso huyu mtu alikuwa anasubiriwa sana kuona atafanya nini baada ya wenzake kina Aslay na Beka kuwa wameshasikika sana, na kuna baadhi ya watu walikuwa wanaamini Maromboso ni mkali kuzidi wote pale walipokuwa Yamoto Band, nadhani na Fella amewaingiza chaka WCB wakaamini hivyo, ila kwa hizi nyimbo 2 alizotoa sijaona hata mmoja unaostua, ni nyimbo za kawaida sana 'beyond expectations', sidhani kama anaweza toboa kwa nyimbo za namna hii, unajua nyimbo nzuri ni kama pembe la ng'ombe (halifichiki), Aslay kipindi ameanza kutoa nyimbo zake alikuwa hata hapeleki Clouds, anaweka U-Tube tu then mitaa inaongea, hili promo wanalompa sahivi wamedandia tu baada ya kuona dogo ana impact kubwa.
So kama Mbosso angekuwa anatoa vitu vikali hata bila ya promo la Clouds angetoboa tu.
Kwa upande wangu hapa kwa Lavalava na Mbosso WCB na 'Mendes' wao wamefanya usajili mbovu, wangemsajili Aslay wangepiga hela mno