Waziri wa Ulinzi: JWTZ si sehemu ya Siasa, ni taasisi mahsusi kwa kazi mahsusi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,810
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena L. Tax amesema Migogoro ya ardhi inayohusisha maeneo ya Jeshi inapaswa kutatuliwa kwa mashauriano kwa kufuata Sheria zilizopo na si Kisiasa

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2024/25 amesema, maeneo ya Jeshi ni maalum kwa shughuli za Kijeshi ikiwemo Ulinzi wa Taifa na hivyo Viongozi na Wananchi wanapatakiwa kuyalinda ili kuepuka Migogoro isiyo ya lazima
Your browser is not able to display this video.
 
Mheshimiwa Stergromena Tax mama makini na mwenye ucheshi ktk kazi makini umesema na kuongea ktk mazingira ya kimsingi na kijamii kwa nyanja Pana sana kongole mama Mungu akujalie binti shupavu kama wewe Mheshimiwa , maana umri ni namba na haziongopi ukifika wakt bas ainuke malkia kama wewe kongole ... Tusahau Mungu ndie mweza na kiongozi mwema makes ya kibinadamu yapo no one is perfect 👌
 
Nimeamini leo kwamba jeshi hakuna siasa,wakati akihojiwa Msemaji wa jeshi la wananchi Kanali Gaudentius Gervas Ilonda Mtangazaji alimuuliza Kuhusu Binti aliyebakwa na wanajeshi lakini kabla hata hajamaliza kuuliza wakaweka tangazo kisha tangazo lilivyoisha swali likaja jingine na mahojiano yakaishia hapo hapo wakafunga kipindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…