Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, amepokelewa wizarani. Aanza kazi rasmi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,714
13,464
WAZIRI WA UJENZI MHE. ABDALLAH ULEGA AANZA KAZI, ASISITIZA USHIRIKIANO
IMG-20241211-WA0013.jpg

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Abdallah Ulega, amepokelewa wizarani na kulakiwa na watumishi wa Wizara, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour na watendaji na wakuu wa taasisi na kusisitiza ushirikiano.

Mapokezi hayo yamefanyika leo Jumatano tarehe 11 Desemba, 2024, katika ofisi za makao makuu ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) jijini Dar es Salaam.
IMG-20241211-WA0043(1).jpg

Akizungumza mara baada ya kuwasili, Mheshimiwa Waziri Ulega amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini na kumteua kuwa Waziri wa Ujenzi ambapo ameahidi utumishi wa uadilifu, uaminifu na kufanya kazi bila kuchoka.
IMG-20241211-WA0041.jpg

"Mafanikio ya Watanzania yanategemea sana ujenzi wa miundombinu bora ya barabara, viwanja vya ndege, vivuko na nyumba za gharama nafuu, hivyo tukiwekeza kikamilifu katika maeneo hayo, tutachochea ukuaji wa uchumi na maendeleleo ya watu" amesema Mhe. Ulega.

Sambamba na hilo, ameomba kupewa ushirikiano wa kutosha utakaomwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kama alivyoaminiwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amemshukuru pia, Katibu Mkuu na watumishi wa Wizara kwa ujumla wao kwa mapokezi mazuri, waliyompa mara tu baada ya kuwasili.
IMG-20241211-WA0033.jpg

Mapema akimkaribisha kuzungumza na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Mhandisi Aisha Amour amesema, Wizara ina taasisi zipatazo 10 ambazo zimejikita katika kuhakikisha sekta ya ujenzi nchini inakua na kutoa fursa za ajira ambazo ni Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa Majengo (TBA), Wakala Ufundi na Umeme (TEMESA), Mfuko wa Barabara (RFB) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).
IMG-20241211-WA0035.jpg

Taasisi nyingine ni
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) na Vikosi vya Ujenzi.
IMG-20241211-WA0029.jpg

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta, akiongea kwa niaba ya wenzake amemuahidi Waziri Ulega ushirikiano ili kutimiza malengo na matarajio ya Mheshimiwa Rais na Watanzania kwa ujumla.
IMG-20241211-WA0027.jpg

Hatua hii inafuatia uteuzi uliofanywa na Rais Dkt. Samia hivi karibuni ambapo alimteua Mhe. Abdallah Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi.
IMG-20241211-WA0015.jpg
IMG-20241211-WA0017.jpg
IMG-20241211-WA0019.jpg
IMG-20241211-WA0023.jpg
IMG-20241211-WA0025.jpg
IMG-20241211-WA0021.jpg
IMG-20241211-WA0031.jpg
IMG-20241211-WA0033.jpg
IMG-20241211-WA0035.jpg
IMG-20241211-WA0037.jpg
 
Back
Top Bottom