M'bang'ang'walu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2015
- 631
- 437
Mkuu umeua! hao wanawalaumu wahindi watuambie wao wana ufahamu gani kuhusu viongozi wa nchi nyingine. Watu hawaelewi kwamba hii Tanzania kuna watu wa sehemu nyingine hapa duniani hawaielewi kabisaUnaweza ukadhani hilo limetokea kwa bahati mbaya,lakini ni ukweli uliodhahiri kuwa pamoja na kuwa BALOZI Mahiga ni mmoja wa viongozi ninaowakubari sana,lakini amepewa uongozi na kiongozi asiyejuwa umuhimu wa "Diplomasia ya nje"
Kama kiongozi wa nchi hana mafungamano na jumuia za kimataifa na amefuta vibali vyote vya kusafiri nje ya nchi,unatarajia mataifa ya nje yatumie "njozi" kuufahamu uongozi wa serikali ya awamu ya tano?Ziara pekee aliyoifanya nje ya nchi ni ile ya kwenda Rwanda "kupokea Zawadi" ya ng'ombe watano,baada ya hapo hakuna juhudi zozote zifanywazo na serikali hii ya kufungua mipaka ya ushirikiano wa kimataifa sasa nchi iliyoamua yenyewe "kujifungia ndani na kukataa mahusiano yoyote na mataifa ya nje",nani atajipa kazi ya kujuwa viongozi wa Taifa letu kama wenye dhamana ya kufanya hivyo wamepigwa " ban" ?
Tumekuwa mabingwa wa kuwakosoa wenzetu ambao makosa yao yamesababishwa na sisi wenyewe kwa kushindwa kuitumia diplomasia vizuri.Kama tatizo ni Wahindi kutowafahamu viongozi wa awamu ya tano,mbona na wetu ni mabingwa wa kutowafahamu watu mashuhuri wa dunia hii? Si tuliambiwa Saddam Hussein ni Rais wa Kuwait,au mmesahau,acha twende hivyo hivyo.