Waziri wa Maji: Mradi umekamilika, tatizo la maji Dar limekwisha rasmi

Kinyerezi hakuna maji, dawasco hawajafika kabisa hivyo akiongea tatizo la maji limeisha ni upuuzi, Dar kubwa sio obay na masaki tu. Watu wanataka maji yavutwe kwao ila bado hawajapata, hivyo shida bado ipo.
Afadhali umesema wewe kutoka CCM! Wengine tukisema mawaziri wa mwendokasi tunaitwa wachochezi! Anasema tatizo la maji Dar limeisha, sijui mipaka ya Dar kwake yeye ni ipi? Tusaidie ndugu labda uko jikoni kwenye vikao vya CCM. Waanze mtandao wa mabomba sehemu zingine ambazo zina watu wengi kama Mbagala etc
 
Kwa Serikali hii yenye sera uchwara hii kauli haina ukweli hata kidogo. Ukifanyika utafiti katika vitongoji mbali mbali vya jiji la Dar tutagundua kwamba tatizo la maji bado liko pale pale.
Mimi naona kweli tatizo la maji kisiasa limeisha ila ki uhalisia...kazi wanayo kupeleka miundombinu ya maji has a sehemu zenye idadi kubwa ya watu. Lakini kama tatizo ni kwa viongozi wa serikali, hapo sawa tatizo limeisha
 
siku akiweza kuwapa maji wakazi wa Goba, Kimara, Kitunda, Mbagala na Kigamboni at least tutaanza kuamini maji yapo Dar...lakini kwa sasa Dar maji hakuna na ndio historia yenyewe
 
Mkazi wa mjini anatumia sio ya chini lita 100 hadi 150 kwa siku(kuoga,kufua, kuosha vyombo, choo cha flush etc) Jiji la Dar linao wakazi wasio pungua milioni nne na nusu. Hivo mahitaji ya maji dar sio chini ya lita milioni 450 kwa siku.
 
Jamani hata sisi wakazi wa Mbweni hakuna maji tunapata shida, waziri angalieni na Mbweni
 
Kama ni hivyo basi hongera zao, ila wasisahau kwamba kuna mikoa mingine ambayo maji ni shida.
 
Back
Top Bottom