Waziri Tabia Mwita: Walioshiriki Samia Fashion Festival 2024 wawezeshwe kulinda vipaji vyao

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,104
2,636
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amewaagiza Viongozi wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni kuhakikisha Wanawawezesha Vijana walioshiriki katika Tamasha la Samia Fashion Fastival 2024 ili kulinda na kuendeleza vipaji vyao.

Ameyaswma hayo katika Tamasha la Samia Fation Fastival 2024 huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege.
1733125678781.png
Amesema Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameweka Sh. Bilioni 36 kwa ajili ya kuwawezesha Vijana, Wanawake na Wenye ulemavu.

Aidha amewataka Wasanii hao wa Mitindo kutoka Zanzibar kujiunga pamoja ili waweze kuwezeshwa kwa urahisi.

"Kuna Vijana wengi wadogo wanavipaji na vitu vikubwa, tusipo wawezesha wanadumaa na wanawacha lakini tukiwawezesha watakuja juu na watawanyanyua na wenzao "alisema Waziri Tabia.
1733125705645.png
Hata hivyo amesema Wizara imelipokea kwa mikono miwili Tamasha hilo na kuahidi kuchukuwa asilimia 50 ya maandalizi yake kwa misimu ijayo pamoja na kutoa lakini 5 kwa Washindi wa 5 wa mwanzo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amesema Wananchi wa Zanzibar wanapenda sana Mavazi lakini hawana ubunifu wa kutosha.

Hivyo kufanyika kwa Tamasha hilo, litasaidia kuongeza ubunifu kwa Vijana wa Zanzibar.
1733125728835.png
Aidha amesema sekta ya ubunifu ni muhimu sana kwani inatoa fursa mbalimbali ikiwemo ajira kwa Vijana na kuahidi kushirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita katika kuwavezeaha Wabunifu wa Mitindo Nchini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar Juma Choum Juma amesema Tamasha hilo limekuwa zuri kwani limezingatia Mila, Silka na Tamaduni za Mzanzibar.
1733125746432.png
Nae Mwanzilishi na Muandaaji wa Tamasha la Samia fashion festival 2024 (Ubunifu na stara Zanzibar) Khadija Mwanamboka amesema lengo la kuandàa Tamasha hilo ni kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan kutokana na anavyowajli Wabunifu.
 
Back
Top Bottom