ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,123
- 68,586
Mkuu tafuta pesa hakuna maisha magumuHata Museveni siku moja alisema, "Uganda maisha rahisi hata Mjiinga anaweza kuishi"
Siku hizi amekuwa ni mropokaji sana. Nadhani amevimbiwa.Duu mwenye shibe hawezi muonea huruma mwenye njaa, haya sawa.
Bodaboda sio kaziSiku moja abadilishane hiyo kazi yake ya ubunge na uwaziri, na bodaboda mwenye elimu ya chuo kikuu walau kwa wiki tu. Halafu aje atoe mrejesho.
Ajiuzulu Ili iwaje?Huyu mzee ni mjinga sn, kwanini yeye asijihuzulu arudi huku tufanye kazi tena yeye tayari ana mtaji?
Mkuu tafuta pesa maisha sio magumuDuh hawa watu walioshiba na kusaza ndo kauli zao hizo siku zote kwahiyo anataka kusema Watanzania hawatafuti pesa ? Posho, mshahara na marupurupu anayopokea kwa nafasi yake anaona wengine hawatafuti pesa Mwela Mwenye shibe hamuoni Mwenye njaa.
Kabisa ndio aone hali inavyokuwa.Siku moja abadilishane hiyo kazi yake ya ubunge na uwaziri, na bodaboda mwenye elimu ya chuo kikuu walau kwa wiki tu. Halafu aje atoe mrejesho.
Na kile kichwa anavyokiwekaga upande sijui ni mapozi au ndivyo alivyo! Hapa ndiyo neelewa hata mwanaye aliwahi tukana askari kumbe tabia katoa kwa Baba yake.Siku hizi amekuwa ni mropokaji sana. Nadhani amevimbiwa.
Nyie ndio Dullah Huwa anawaambia mjiongeze, uwe welder harafu muuza mchicha π€£π€£π€£π€£Haya nina ofisi ya welding na mgao huu wa umeme na hapo hapo kila wiki linatakiwa rejesho benki..nafanyeje kazi??
Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
Mbona huyu Mhe. anaemkeDaa amesahau alivyofuria kipindi fulani Magu amemuweka Benchi. Mpaka akawa anampandisha mchepuko wake Bajaji kumleta ghetoni kwake hapo kisasa nyumba mia 300!
Kazi zenyewe za kufanya ziko wapi?.Kama Kuna rafiki yake humu,amwambie kuwa cha Arusha ni kikali asitumie sana!Boniface Simbachawene amewachana live watu waache visingizio na watafute pesa kwa kufanya kazi zaidi kwani maisha sio magumu Bali mahitaji ya pesa yameongezeka.
My Take
Watu waambiwe ukweli hakuna kupakwa mafuta Kwa mgongo wa chupa.
=====
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha.
Amesema ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili aweze kupata fedha za kumuwezesha kumudu huduma muhimu katika jamii.
Mhe. Simbachawene ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbuga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.
"Ukiwa huna fedha ikitokea umeumwa, utashindwa kupata matibabu na kuweza kuhatarisha uhai wako, hivyo ni bora kila mmoja wetu akahakikisha anafanya kazi ili apate fedha za kumudu mahitaji muhimu," amesema Waziri Simbachawene.
Amesema kila mwananchi kwa nafasi yake ni muhimu akahakikisha anajikita katika kuzalisha mali ili aweze kupata fedha.
Amefafanua kuwa hakuna maisha magumu kama inavyodaiwa na watu wengi isipokuwa mahitaji ya fedha yameongezeka kutokana na kukua kwa maendeleo.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kukaa bila kufanya kazi badala yake waitumie ardhi yenye rutuba waliyojaaliwa kuwa nayo kwa ajili ya shughuli za kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Chanzo: EA Radio