Waziri Simbachawene: Watanzania fanyeni kazi na mtafute pesa. Maisha sio Magumu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
59,564
70,214
Boniface Simbachawene amewachana live watu waache visingizio na watafute pesa kwa kufanya kazi zaidi kwani maisha sio magumu Bali mahitaji ya pesa yameongezeka.

My Take
Watu waambiwe ukweli hakuna kupakwa mafuta Kwa mgongo wa chupa.😂😂

=====

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha.

Amesema ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili aweze kupata fedha za kumuwezesha kumudu huduma muhimu katika jamii.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbuga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.

"Ukiwa huna fedha ikitokea umeumwa, utashindwa kupata matibabu na kuweza kuhatarisha uhai wako, hivyo ni bora kila mmoja wetu akahakikisha anafanya kazi ili apate fedha za kumudu mahitaji muhimu," amesema Waziri Simbachawene.

Amesema kila mwananchi kwa nafasi yake ni muhimu akahakikisha anajikita katika kuzalisha mali ili aweze kupata fedha.

Amefafanua kuwa hakuna maisha magumu kama inavyodaiwa na watu wengi isipokuwa mahitaji ya fedha yameongezeka kutokana na kukua kwa maendeleo.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kukaa bila kufanya kazi badala yake waitumie ardhi yenye rutuba waliyojaaliwa kuwa nayo kwa ajili ya shughuli za kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Chanzo: EA Radio
 
Duh hawa watu walioshiba na kusaza ndo kauli zao hizo siku zote kwahiyo anataka kusema Watanzania hawatafuti pesa ? Posho, mshahara na marupurupu anayopokea kwa nafasi yake anaona wengine hawatafuti pesa kweli mwenye shibe hamuoni mwenye njaa.
 
Duh hawa watu walioshiba na kusaza ndo kauli zao hizo siku zote kwahiyo anataka kusema Watanzania hawatafuti pesa ? Posho, mshahara na marupurupu anayopokea kwa nafasi yake anaona wengine hawatafuti pesa Mwela Mwenye shibe hamuoni Mwenye njaa.
Mkuu tafuta pesa maisha sio magumu
 
Boniface Simbachawene amewachana live watu waache visingizio na watafute pesa kwa kufanya kazi zaidi kwani maisha sio magumu Bali mahitaji ya pesa yameongezeka.

My Take
Watu waambiwe ukweli hakuna kupakwa mafuta Kwa mgongo wa chupa.

=====

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujiingizia kipato cha kuweza kumudu gharama za maisha.

Amesema ni wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili aweze kupata fedha za kumuwezesha kumudu huduma muhimu katika jamii.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbuga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo lake.

"Ukiwa huna fedha ikitokea umeumwa, utashindwa kupata matibabu na kuweza kuhatarisha uhai wako, hivyo ni bora kila mmoja wetu akahakikisha anafanya kazi ili apate fedha za kumudu mahitaji muhimu," amesema Waziri Simbachawene.

Amesema kila mwananchi kwa nafasi yake ni muhimu akahakikisha anajikita katika kuzalisha mali ili aweze kupata fedha.

Amefafanua kuwa hakuna maisha magumu kama inavyodaiwa na watu wengi isipokuwa mahitaji ya fedha yameongezeka kutokana na kukua kwa maendeleo.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kukaa bila kufanya kazi badala yake waitumie ardhi yenye rutuba waliyojaaliwa kuwa nayo kwa ajili ya shughuli za kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Chanzo: EA Radio
Kazi zenyewe za kufanya ziko wapi?.Kama Kuna rafiki yake humu,amwambie kuwa cha Arusha ni kikali asitumie sana!
 
Back
Top Bottom