Waziri Ndalichako hana jipya, asema 'grades' za ufaulu zitabaki kama zilivyo!

Sera sio mbovu tatizo haijatekelezwa kwa kiwango cha aslimia mia. Nadhani hadi sasa hata 50 % ya utekelezaji wa sera hiyo haujaafikiwa. Pia sera haitamki grades. Tumpe muda aisimamie sera hiyo. Kwa taarifa tu, uandaaji wa sera huhusisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wasomi, sasa unavosema wasomi wanaipinga hiyo sera, je ni wasomi gani? Si ajabu ww uliyeweka hili bandiko hapa hata hiyo sera hujawahi kuiona wala kuisoma. Unaandika mambo kwa hisia na mhemko wa kisiasa, na sio weledi wa mambo
 
There
Watanzania tuache kuwa na maono ya kuku (chicken vision) na kuwa na maono ya tai (eagle vision).

Kila nikisoma post Kama hii huwa najiuliza level ya elimu??? aim ya bandiko hili???? Walengwa nk

Nashauri Kama kweli tunataka kuipa hadhi JF na tunataka policy makers wafanye reference humu, basi tubadili tabia.

Naamini unaweza kwenda mbali zaidi kwa kutuambia yafuatayo:-
1. Kwanini grades zilibadilishwa???
2. Je visababisho tajwa vimeshughulikiwa???
3. Kama bado je unashauri nini kifanyike huku ukiorodhesha kila sababu na mapendekezo yake.
4. Je turudi kwenye grades za awali? Nini faida na hasara.

Tubebe elimu ktk uzalendo wa asilimia 100% maana watoto wetu wanahitaji elimu kuliko mnavyofikiri.

Queen Esther

tanzania
Ningemshangaa SANA kubadilisha grading system . Hakuna tatizo Lolote na mfumo huo cha msingi NI kusimamia viwango .
 
Un
Waziri pekee wa serikali ya rais John Magufuli aliyenivutia sasa ameanza kunivunja moyo baada ya kuendeleza yale yaliyozorotesha elimu ya Tanzania, nimethibitisha.

Waziri Joyce Ndalichako anayesimamia elimu na mafunzo ya ufundi amebainisha kuwa ataisimamia sera mpya ya elimu iliyoanzishwa hivi karibuni.

Sera hiyo ndiyo iliyobadili kabisa mfumo wa upangaji matokeo na udahili wa wanafunzi kwa elimu ya juu, vyuo na shule za sekondari ambayo inapingwa vikali na wasomi.

Sera mpya ya elimu inaelezwa kuwa ni mbaya na haikidhi viwango vya ubora katika elimu. Miongoni mwa watu wengine waliopewa jukumu la kusimamia elimu na kuiulia mbali ni Joseph Mungai ambaye aliisambaratisha vibaya elimu ya sayansi kwa shule za msingi na sekondari.[/QUOTE
Waziri pekee wa serikali ya rais John Magufuli aliyenivutia sasa ameanza kunivunja moyo baada ya kuendeleza yale yaliyozorotesha elimu ya Tanzania, nimethibitisha.

Waziri Joyce Ndalichako anayesimamia elimu na mafunzo ya ufundi amebainisha kuwa ataisimamia sera mpya ya elimu iliyoanzishwa hivi karibuni.

Sera hiyo ndiyo iliyobadili kabisa mfumo wa upangaji matokeo na udahili wa wanafunzi kwa elimu ya juu, vyuo na shule za sekondari ambayo inapingwa vikali na wasomi.

Sera mpya ya elimu inaelezwa kuwa ni mbaya na haikidhi viwango vya ubora katika elimu. Miongoni mwa watu wengine waliopewa jukumu la kusimamia elimu na kuiulia mbali ni Joseph Mungai ambaye aliisambaratisha vibaya elimu ya sayansi kwa shule za msingi na sekondari.
mkuu unAweza nieleza tatizo la mfumo huo ???
 
Kwanini Watoa mada wengi humu JF wanakurupuka wakati Waku creat thread zao kwanini?

Kwanini wachangiaji wengi humu JF wanakurupuka wakati wa kuchangia bila kujua anachangia nini?

Sikuhizi ufahari wa JF Ni kucreat thread nakupata comment nyingi si ndio

Kwanini tunaifanya JF kama insta,au Groups zetu za whatsapp? kwanini tuifanya kama FACEBOOK

Walio andika Home of great thinkers walikuwa wajinga?

Mtu unavimbiwa pilau ya mwaka mpya mbio mbio kuja kupost na kuanza kumtuhumu mtu bila aibu watu wanachangia kumtuhumu

Upo JF hujui hata SERA YA ELIMU? kweli kusema atasimamia Sera ya elimu ndo kasema kuwa hata badirisha grades upo serious na povu linakutoka

Mtu hata kazini hana mda mrefu unatka kila kitu akifanye siku moja hata Vikao hajafanya ndo kwanza katibu wake jana kateuliwa watu mapovu hayooooo

Msituharibie JF FAanya utafiki kabla ya kupost
 
Inawezekana uko sahihi kabisa. Je kitu hicho kinaweza kufanyiwa Kama ulivyoshauri ndani ya wiki moja??? Au una shida binafsi na huyu mama??

Queen Esther

Hv we jamaa ina maana hujui ubovu wa elimu ya tz hadi unaandika mineno yote hii et kuisifu elimu iliyopo..
Sasa katka viswali vyako ulivoulza ngoja nikujibu baadhi..
1. Sabab ya kubadilisha grade ilikuwa ya kisiasa yaan ionekane wanafunz wanafaulu kumbe hola ndo hayo ya kutojua kusoma na kuandika
2. Ndio kurudisha zile grade za zamani ni sawa ili wanafunzi na wanasiasa wajione wanavofeli kwa kushindwa kumit ufaulu bora
3. Cha kufanyika ni kuukataa mitaala yote iliyopo na kuunda mtaala mpya utakaoshirikisha wadau nikiwemo na mm ili tuweke mambo ya msingi ambayo hakuna haja ya kusoma shule mda mrefu na kupoteza mda hafu mwishon mtu anatoka hana ujuzi wowote. Vyuo vya ufundi virejeshwe na ndio viwe vingi, haya ma University ni mbwembwe tu na usharobaro hakuna kitu.
University ziwepo chache kwa wasongo ila vyuo vya kati ndo viwe vingi, pia tutengeneze mtaala utakaomfanya mwanafunzi asikariri bali aelewe na akitoka atoke na ujuzi na sio max nzuri za kudesa
 
Inawezekana uko sahihi kabisa. Je kitu hicho kinaweza kufanyiwa Kama ulivyoshauri ndani ya wiki moja??? Au una shida binafsi na huyu mama??

Queen Esther

Sasa kama unakubali haya mapungufu kwanin unaunga mkono huu upuuzi..
Ndio itz possible kufanya changes even a second.. Ni kuamua tu...
Let m tell u, walioko sehemu za maamuz hawajaamua kutukwamua bado wanapiga blabla... Lait kama ungelijua hili usingeshoboka kusifia hizi blabla..
Kitendo cha mtu kukubali current grade pass ziendelee kutumika inatia shaka sana dats y hatuamini juu ya mabadiliko yanayotajwa kwa mgongo wa chupa
 
Yaani shida hii nchi kila mtu anajua kila kitu, hata wa vijiweni ni wataalam kuliko mhe prof Ndalichako.
Hongera zenu
Acha utoto na ufiche ujinga wako, hv unafikiri ukichaguliwa kushika wadhifa fulani inamaana una akil kulko wengine..??
Wajinga ndo mnaamini hvo... Kwa taarifa yako huku kitaa unapopadharau ndo wamejaa wazalendo kulko wa huko juu..
 
Sijajua watu wangapi wameisoma hiyo sera ya elimu 2014.
Naona watu wanaongelea vitu tofauti na vilivyomo.
 
Hata wiki bado mmeishaanza kumkeuka daah!! Dr.Magufuli alisikia kilio chenu kupitia JF kamchagua leo tena hatakiwi Bavicha bana.
 
Mbona hizo grades (GPA) ndo zinazorumiwa ss kimataifa! Mambo ya division yashapitwa na wakati badiliken, achanen na mawazo mgando
 
Yaleyale!

Inachekesha jitu lililosoma chuo kikuu likatumia mfumo wa GPA kusema haelewi mfumo wa GPA unaotumia sekondari. inashangaza unakuta mtu kaandika kuwa zimewekwa GPA ili aliyepata GPA ya 1.7 aonekane amefaulu. Hivi ni chuo gani duniani GPA ya 1.7 ni kiwango kizuri cha ufaulu?

Haijalishi marks ziko katika mfumo gani, u can only fool those who do not understand your passing grades sio wanaoelewa. Na hauwezi mdanganya yoyote duniani kuhusu ufaulu wako kwa kusema GPA ya 1.7 ni nzuri na bora.

Halafu mtu huyo anayepinga hachelewi kurudi na kusema kuwa tuwaige marekani wao wana mfumo mzuri, wakati nao wanatumia hizo hizo GPA.

Muwe mnatafuta vitu vya msingi kupinga!
 
Waziri pekee wa serikali ya rais John Magufuli aliyenivutia sasa ameanza kunivunja moyo baada ya kuendeleza yale yaliyozorotesha elimu ya Tanzania, nimethibitisha.

Waziri Joyce Ndalichako anayesimamia elimu na mafunzo ya ufundi amebainisha kuwa ataisimamia sera mpya ya elimu iliyoanzishwa hivi karibuni.

Sera hiyo ndiyo iliyobadili kabisa mfumo wa upangaji matokeo na udahili wa wanafunzi kwa elimu ya juu, vyuo na shule za sekondari ambayo inapingwa vikali na wasomi.

Sera mpya ya elimu inaelezwa kuwa ni mbaya na haikidhi viwango vya ubora katika elimu. Miongoni mwa watu wengine waliopewa jukumu la kusimamia elimu na kuiulia mbali ni Joseph Mungai ambaye aliisambaratisha vibaya elimu ya sayansi kwa shule za msingi na sekondari.
Akili ya UKAWA inakusumbua, hata week haijaisha umeanza kulalamika?
 
Huyu mama anaogopa sabatical leave nyingine. Chezea ccm wewe!? Angalia Tido Muhando alichofanyiwa kwa kupingana nao juu ya kufuta kipindi cha mchakato majimboni TBC1 2010. Linganisha na waliokuwa watiifu akina Shaban Kisu.
Ndalichako kapaona.....fisiem ni ile ile.
 
Back
Top Bottom