Waziri Mwijage: Uhaba wa Sukari umetushtukiza

lakini bado siamini kwamba humu tanzania sukari hamna, sukari ipo jamaa wameificha
 
Waziri anashangaza sana kwamba maana yake walikurupuka hivyo hawakujua kwamba wana akiba kiasi gani.Kweli tunaisoma namba.ccm ileile.
 
Waulevini watapita mbali Na huu uzi.Eti wanaanzisha uzi za Lowasa Ili kutuliza mambo.Mh. Mwijage kaongea ukweli.He call spade a spade and not a big spoon.Waulevini mpo.
 
Mhe.Mwijage waziri wa Viwanda amehojiwa na Radio One Radia asubuhi ya leo, kuhusu uhaba wa sukari unaoendelea nchi nzima.
Akijibu kwa kujiamini anasema Uhaba wa Sukari umewashtukiza.Ukizingatia wao ni wapya na ndio wanajipanga.Pia amekazia kuwa uhaba wa sukari umesababishwa na msimu wa uzalishaji kukoma katika viwanda vya sukari!!!....Asante Mwijage kwa kuonyesha rangi halisi ya Serikali yenu
Huyu jamaa kwa aina ya uropokaji huu si ajabu unaweza kuta katwanga pombe maanake wote wale ni walevi ata mamuzi yao ni ya kilevi.
 
Shida ya sukari miezi 3 faraja ya miaka ijayo litapita tu
Nguvu ya serikali na wafanyabiaahara za magendo
 
Mhe.Mwijage waziri wa Viwanda amehojiwa na Radio One Radia asubuhi ya leo, kuhusu uhaba wa sukari unaoendelea nchi nzima.
Akijibu kwa kujiamini anasema Uhaba wa Sukari umewashtukiza.Ukizingatia wao ni wapya na ndio wanajipanga.Pia amekazia kuwa uhaba wa sukari umesababishwa na msimu wa uzalishaji kukoma katika viwanda vya sukari!!!....Asante Mwijage kwa kuonyesha rangi halisi ya Serikali yenu

Siyo kweli kuwa wamestukizwa ila ni papara za utendaji wa mihemko kwani kabla ya kuzuia sukari ya nje hakukuwa na tatizo la sukari sasa kwa kuwa maamuzi yanapitishwa bila kufanya uchunguzi matokeo yake makazuia sukari toka nje wakati ninyi hamzalishi. Hii issue ilikuwa rahisi sana.

Mmekosea kuzuia sukari na kumetokea uhaba, haraka haraka mngeruhusu sukari iingizwe hadi viwanda vyetu vitakapo anza kazi na kutosheleza soko. Sasa badala yake mmeanza kuvamia maghala ya wafanyabiashara. Mkifika mnakuta sukari na bidhaa nyingine kama ngano lakini ninyi mnakamata sukari eti imefichwa.

Hakuna cha kusitukizwa hapo ila ni maamuzi ya kukurupuka ndio yamesababisha hali kuwa hii. Wananchi ndio tunaumia ninyi huko juu hamnunui sukari, nguo wala chakula bado hamuoni umuhimu wa kuruhusu sukari iingizwe.
 
Mara ya mwisho kusikia na kuona Uhaba wa Sukari ni utawala wa hayati baba wa taifa mwalimu Nyerere sijui Magufuli kamkosea nini Mungu!
Hajamkosea Mungu mkuu, kumbuka maneno yanaumba wengii walitamba baada ya mwalimu rais ni Magufuli waki maanisha awamu tatu nyingine hakukuwa na marais, sasa acha yale ya mwalimu yajirudie ndio waliyo yataka, tunaweza kujikuta tunaingia vitani pia na nchi yoyote jirani tumpime na uwezo wake kivita.
 
Mawaziri hwa kitwanga lization, tutasikia mengi na kushuhudia vituko vya kutosha, uhaba umestukiza?! tehtehthee kama sio wao walisthukiza kuzuia sukari hii hali isingekuwepo.
 
Sukari hanasa! Kwanza nayo inachelewesha watu kuwahi kazini! Vijiwe vya kahawa sasa hakukariki kashata walizokizitegemea kuzimulia uchungu ili waendelee na porojo hazilelei!

Kwanza ikipatikana kirahisi inatumiwa hovyo kikombe kimoja vijiko kuanzia 6 tena watu wengine hadi kwenye maharage wanatia hatimaye wanaugua na lawama kwa serikali! Baadhi ya waTz sio wazalendo!

Kazi kukosoana tu kwanza ni majipu nao hawa! Mara waitajetaje Escrow,kivuko feki,lugumi,sukari,ulevi n.k. Badala ya kujadili mambo ya maendeleo bhana! Hivi hamujui hii ni awamu ya hapa kazi tu.

Nkijaribu kuwa pro lumumba jamani sijui nimepetia!, hahahahahahaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom