Waziri Mwakyembe: Hakuna sheria inayokataa mikutano ya kisiasa baada ya Uchaguzi

Haya ni matokeo ya tishio la kumvua madaraka bwana yule kwa kukiuka katiba na wala si sababu nyingine.

Vitendo vya kuvunja katiba vimekuwa vingi na sasa wameona hatari iliyo mbele yao.

Kama sababu siyo hiyo basi watakuwa wameona hili agizo linawaathiri hata wao wenyewe kama chama tawala na hivyo wanaanza kuikana kauli yao.

Najiuliza kama Mwakyembe anaweza kuongea jambo hili kama halikujadiliwa kwenye cabinet na kupitishwa(mtazamo wangu).
 
Mwakyembe kuna muda kichwa kinafanya kazi vizuri kama mtanzania na kuna muda unajitoa Ufahamu kama vile ujasoma kitu chochote acha hizo brother Tanzania ni yetu sote vyeo ni vitu vya kupita mwambie na uncle na makonda hapa Duniani tunapita tutasifiwa kwa mazuri au kwa mabaya tuliyotenda sio mbwembwe mnazofanya kwe hii awamu 5 mnaboa kweli kweli na mungu anawaona
 
Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Amesema, Tanzania haina sheria wala kanuni zinazo wadhibiti na kuwasimamia wanasiasa kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao jambo ambalo limekuwa likileta mvutano akitolea mfano zuio la kuendesha shuguli za kisiasa nchini hadi uchaguzi wa mwaka 2020 ambao unalalamikiwa na vyama vya upinzani.

View attachment 470562

Chanzo: EATV
Kama kweli alitamka haya kesho hana kazi. kwa Dikteta magufuri hizi ndizo kauli zinazomuudhi kutoa tafsiri sahihi ya katiba hii mbovu tuliyonayo
 
Labda atangaze kuwa mikutano imeruhusiwa mbali na hapo hakutakucha kabla jogoo hajawika Mara tatu atakua ameshajikana Mara tatu.
 
Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Amesema, Tanzania haina sheria wala kanuni zinazo wadhibiti na kuwasimamia wanasiasa kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao jambo ambalo limekuwa likileta mvutano akitolea mfano zuio la kuendesha shuguli za kisiasa nchini hadi uchaguzi wa mwaka 2020 ambao unalalamikiwa na vyama vya upinzani.

View attachment 470562

Chanzo: EATV
Huyu toka abunduke ngozi naona kama kadata,kesho utasikia ooooo magazeti yanaleta uchochezi
 
Back
Top Bottom