Kuelekea 2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa majibu ya matukio ya kupotea na utekaji watu yanaendelea Nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,774
117,228
Waziri Mkuu Akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, Bunge la kumi na mbili mkutano wa 16 kikao cha 3 tarehe 29 Agosti, 2024

Update....

Waziri Mkuu Ametoa majibu ya matukio ya utekaji yanaendelea

Nataka nieleze kwamba tunapoilinda Nchi ni wajibu wetu Watanzania wote kwa kushirikiana na vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama. Tunavyo vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini vyenye jukumu la kupokea taarifa mbalimbali zinazoonyesha uvunjifu wa amani popote pale na jukumu lao wanapokea taarifa ni kuhakikisha wanafanya uchunguzi na uchunguzi utakao baini waliotenda makosa wanachukuliwa hatua kwa kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Ni wahakikishe Watanzania kwamba suala la Ulinzi na Usalama bado lipo mikononi mwetu pamoja na vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama. Jukumu letu ni kuhakikisha tunasaidia Vyombo vya Ulinzi kwa kutoa taarifa zozote zile ambazo zinaleta tishio la amani katika Nchi ili kuvisaidia vyombo vyetu viweze kuchukua tahadhari na hatua stahiki ili kuwabaini wale wote ambao wana sababisha kutokuwepo kwa amani Nchi yetu.

Lakini pia nitoe wito kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuendelea na wajibu wao wa kuhakikisha kwamba kila taarifa inayopatikana lazima ifanyiwe uchunguzi lakini pia nakubaini wale wote wanao husika kama wanapatikana wachukuliwe hatua mara moja.

Soma Pia:
Majibu ya Waziri Mkuu kuhusu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kukamata wananchi bila sababu ya msingi

Amesema ni kweli baadhi ya watala kwenye maeneo yao wanazo sheria ambazo zinawarusu kuhakikisha kwamba hali ya utulivu kwenye maeneo yao inaimalika. Sheria hile inayomruhusu Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya kumkamata mwananchi au mtu yoyote yule na kumuweka ndani, haikulenga kama baadhi wanaweza kuwa wanaitumia.

Lengo ni katika kuhakikisha kwamba mazingira hayo usitokee uvunjivu wa amani mkubwa na kwahiyo anaweza kutumia sheria hiyo kumuhifadhi mahali ili hali itulie na baadae aweze kutoka na kuendelea na majukumu yake.

Anaweza kuwa tishio lipo kwa Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa mwenyewe anaweza kutumia nafasi hiyo, inaweza jambo hilo kuwa hatari kwa Wananchi anaweza kuitumia nafasi hiyo ili kulinda usalama wa Raia lakini pia hata huyo huyo mwanachi analeta hiyo hoja kulinda usalama wake basi sheria inaweza kutumika kwa yeye kumuondoa eneo lile na kumuhifadhi mahali.

Week mbili tatu zilizopita Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa walitwa hapa mkoa Dodoma kwa semina katika maeneo mbalimbali eneo la sheria hii limezungumzwa sana na wameelishwa sana na tunaamini sasa watakuwa wanaelewa namna ya kutumia sheria hile bila kuleta madhara, chuki miongoni mwao na wananchi bila kuleta mtafaruko katika jamii, ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Soma Pia: Mbunge Kunambi: Baadhi ma RC na ma DC wanakamata wananchi bila sababu ya msingi

Na hata kama wanatumia sheria hii mashariti yake ni msaa 24, ambayo baada ya masaa 24 anatakiwa kutoa taarifa ni kwanini aliyeko ndani kawekwa na kuwezsha chombo husika kuchukua hatua na kama hana jambo lolote anatakiwa baada ya masaa 24 yule ambae yupo polisi anatakiwa aondoke.

 
Back
Top Bottom