Waziri Mkuu Azindua Kiwanda Cha Kuchakata Muhogo

Wanunuzi wapo kweli mfano nikalima heka mia tatu au mia nne?
Wapo na wana kuja kucheki shamba lako wanakuazima mashine hii ya kuchakata inatumia generator. Hilo lundo lote ni kama saa 1 tu kuchakata.

P1030405.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa akili zetu zinafanya kazi namna gani.

Mchina anataka tulime mhogo, halafu tumuuzie mhogo huo yeye akatengeneze vitu vya thamani kwao. Kwani hawezi kujenga kiwanda hapa, nasi tukapata ajila za watu wetu, na akasafirisha mali iliyotengenezwa ikauzwe huko China?

Kwa nini iwe hivi kila mara? Wao watuuzie vya thamani kubwa, sisi tuwauzie vya thamani ndogo! Tukihitaji 'starch ya mhogo', tukaagize China, 'starch' ileile iliyotokana na mhogo wetu?

Hivyo viwanda vya kutengeneza wanga vina ugumu gani wa kuvijenga na kuviendesha hapa kwetu?

Na tunajigamba tunaandaa uchumi wa viwanda!
Hujazuiwa mkuu
 
Wakuu habari za jioni.
Leo tarehe 22 Machi 2019 kwenye taarifa ya habari ya saa kumi jioni nimemuona Waziri Mkuu akizindua kiwanda cha kuchakata muhogo.

Nafikiri hii ni fursa nzuri kwa wakulima wa zao hili kwa Mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani.

Nami sitaki fursa hii inipite hivyo naomba mwenye taarifa nzuri kuhusu kiwanda hiki anijuze pamoja nawengine wanao zihitaji, hasa taarifa za bei ya muhungo kwa ekari, upatikanaji wa mashamba, pembejeo, mbegu nk.

Natanguliza shukurani zangu za dhati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho ni kiwanda kidogo sana kwa uwekezaji toka nje mpaka kifunguliwe na mtu mzito kama huyo. Labda angekata Utepe Dc au Rc.

Eka 1 ina miche 4000 ya mihogo. inayopandwa. Kama kila shina linatoa mhogo kg 10 utaona ni kg 40,000 kwa eka 1. Yaani tani 40.

Mimi shambani kwangu shina moja mengine yamefika kg 18 mpaka 20.
Nikichukulia wastani wa angalau kg 10 x 4000 x eka 5 nilizolima ni kg 200,000/=

Tani 200 za mhogo mbichi . Kwa hiyo ni kiwanda kidogo. Kama ni kuchakata tan 100 kwa siku. Kwa Wilaya nzima itakuwa shida foleni ndefu labda wakipanue. Wachangiaje wengine naona wanachangia kisiasa. Hali halisi ni tofauti kabisa.

Kuwa na mawazo mbadala sio maanake ni kupinga ila kujaribu kuboresha kwa mawazo tofauti. Kwa mfabo hapa tatizo bi bei ya kununlia mhogo soko lipo.


Nadhani ukiangalia hizi picha utakubali wakulima wa mhogo tupo ila blah blah nyingi kwenye fursa.

Wanataka tuukaushe halafu tuweke kwenye viroba vya 50kg @ na bei ni 280/= akiiufuata ukimpekea ananunua kwa Tshs 300. View attachment 1064932View attachment 1064933

Sent using Jamii Forums mobile app
hii mbegu ni aina gani na ninaweza kuipata.?
 
Back
Top Bottom