Wanabodi,
Nafuatilia Bunge Live kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Nimesikiliza maswali magumu mazito ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe na majibu rahisi na mapesi ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
This leaves much to be desired kuhusu uwezo wa Waziri Mkuu wetu kujibu maswali magumu mazito kwa kutoa majibu rahisi na mapesi.
Maswali yamehusu
1. Sintofahamu ya hali ya usalama
2.Kupotea Kwa Ben Saanane 6 months bila taarifa, tuwaite Scotland Yard Watusaidie?.
3. The right to information ya Bunge Live.
Majibu.
1. Hali ni shwari na vyombo vya ulinzi na usalama viko makini kwenye hili, muhimu ni kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kunapotokea Sintofahamu yoyote.
2. Uchunguzi unaendelea kuhusu kupotea kwa Ben Saanane na Uchunguzi hauna time frame. Tanzania inashirikia na vyombo vya nje ikiwemo Scotland Yard ila vyombo vya ndani vina uwezo, tuviaminie. Uchunguzi ukikamilika, taarifa itatolewa.
3. Bunge Live: Bunge liliisha amua namna ya kutoa habari zake kwa umma.
Waziri Mkuu anapotoa majibu mapesi kwa maswali magumu na majibu rahisi kwa maswali mazito kuhusu hali ya usalama wa raia: Jee ni uwezo mdogo wa kujibu maswali magumu kwa majibu rahisi au ni majibu ya makusudi tuu just for saving faces ya kuilinda serikali pale ambapo serikali haina majibu yards maswali hayo?.
Kitu kizuri kuhusu majibu ya Waziri Mkuu kilichonifurahisha ni jinsi alivyo humble, simple na down to earth kwa kujibu kwa unyenyekevu mkubwa na kuonyesha heshima kwa KUB.
My Take.
1. Kwanza Wabunge wetu wapewe semina ya jinsi ya kuuliza maswali na sio kutoa hutuba. Beating around the bush for too long kunapunguza strength ya swali.
2. Viongozi wafunze kutoe majibu sahihi ya maswali na sio nao kutoa maelezo marefu na wao pia kuhutubia bila concise answers!.
,
Pongezi pia kwa Spika Ndugai kwa uvumilivu wa kuvumilia maelezo mareefu ya wabunge, enzi za Speed and Standards (RIP), there was no room ya hii dilly darling kama hii, wengine maswali waliyaandika na kuuliza ili tuu kuonyesha uwepo wao bungeni.
Kwa mwendo huu, kiukweli kazi bado tunayo na safari bado ni ndefu. Jee tutafika? .
Wasalaam
Alhamisi Njema.
Paskali
Mi sikuona swali lolote zito pale usitake kupotosha watu .. Yote yalioulizwa yalishatolewa majibu. Naona bado mnatamani kuuza sura kwenye screen ili muonekane . Hiyo fursa imeshapotea.