Waziri Mkuu akerwa na Kiwanda cha mbolea cha Minjigu kutumia mifuko inayoonesha ni ya Kenya!

Malighafi inatoka Tanzania?

Malighafi ya kutengenezea microchips za simu Tungstein, Tin, Tuntulum, zinatoka Congo. Kwa hiyo IPHONE ziandikwe anuani ya Lubumbashi?

Tunatoa malighafi, hatutoi mbolea. Mbolea inatoka wapi, hakieleweki, Waziri Mkuu ameng'ang'ania malighafi, malighafi, malighafi...
 
Hapo ni wizi mchana kweupe, nembo ya Kenya hapohapo unauziwa bei juu kwa kuwa ni ya Kenya,
Na ikienda Kenya inakuwa kama imetengenezwa kwao duu jamaa waizi kweli
 
Malighafi inatoka Tanzania?

Malighafi ya kutengenezea microchips za simu Tungstein, Tin, Tuntulum, zinatoka Congo. Kwa hiyo IPHONE ziandikwe anuani ya Lubumbashi?

Tunatoa malighafi, hatutoi mbolea. Mbolea inatoka wapi, hakieleweki, Waziri Mkuu ameng'ang'ania malighafi, malighafi, malighafi...
Tulia kwanza mkuu. Hapo wanatengeneza mbolea complete. Ukinunua mfuko wako hapo kiwandani unakwenda kuweka shambani kwako direct
 
Nimeona sana mkuu, nimeuliza swali hilo ili Watanzania wajifunze kitu - ni hivi: kinacho fanyika pale ni mbinu za kibiashara, kwani Tanzania inapoteza nini?

Mbolea inanununiliwa na Wakenya kutoka Minjingu kama kawaida hisipokuwa nembo tu ndiyo inabadirishwa kwa lengo la kuvutia Wakenya wenzao lakini sisi tunalipwa kama kawaida.

Naona some Members wanawajia juu Wakenya bila ya kutafakari mambo ya biashara, mbona naweza kuagiza communication equipment/hardware kutoka Uchina na kuwambia Wachina wabandike lebo ya Bijampola na made in Bukoba,Tanzania na wakafanya hivyo - wao wabacho jali ni kuuza bidhaa zao, mambo mengine ni secondary - je, Wakenya wange ondoa jina la Minjingu wakaweka jina la Shimo laTewa au Kware Mombasa, mgesema nini?
Uko sahihi ni Mbinu ya Kibiashara lakini unapokuwa unamsaidia mwenzako kutangaza nchi yake huku yako ukiiacha nyuma unakuwa unafanya hapo.?

Mfano, Unafikiri ni Watalii wangapi wamekuja kwa kuangalia Serengeti tu ila wakajikuta wamefika Zanzibar,Mikumi au Hata Milima kilimanjaro.?

Maana yake ni kwamba Unapokuwa unamtangaza Mwenzako hata kama kakulipa ipasavyo unamfanya awe maarufu kuliko wewe matokeo yake kwa umaarufu huo watapata vingi,mfano mkubwa ni hao watalii ambao wataamini Kenya iko vzr zaidi.
Ko hii haitaishia kwenye cement tu mtawapa mwanya wa kujitangaza zaidi huku ninyi mkijirudisha nyuma.

Mfano, Ushajiuliza kwa nn Iphone haziandikwi made in US, ILA made in China na tunajua kabsa ni kampuni ya Marekani.?
 
Yaani mbolea izalishwe Tanzania halafu iwe branded Made in Kenya, kweli? Nyie jamaa sasa hizi sifa...Mheshimiwa Rais hawa chapa viboko kabisa!

========

View attachment 472192

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.

“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.

“Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”

Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.

Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

“Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.

“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”

“Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.

Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.

Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.
Nampongeza PM kwa hatua hiyo. Mikoa kama ya Rukwa na Songwe,sehemu kubwa ya mbolea inayotumika,wananunua kutoka Zambia! Wanadai ya kwetu aidha ni hafifu au haifiki kukidhi mahitaji! Hali kadhalika mbegu mfano za mahindi. Uchunguzi ufanyike,yawezekana ni ujanja huo huo,kuwa ya kwetu inakwenda Zambia,na then inakuwa repacked kwa label zao. This is a serious issue! Hongera tena PM kwa kuliona hilo.
 
Tulia kwanza mkuu. Hapo wanatengeneza mbolea complete. Ukinunua mfuko wako hapo kiwandani unakwenda kuweka shambani kwako direct


Sasa kwa nini Waziri Mkuu anaongelea malighafi, malighafi, malighafi...?
 
Hata Majaliwa ana tatizo. sijaelewa agizo la kuwataka wamwandikie barua Magufuli, sielewi. Ina maana yeye kama Waziri Mkuu hawezi kuchukua hatua? aaaaah! katibua hapo tu!
Hujajua ni kwani nini? Shida ni kwamba hutufukui makaburi hii ni brand hili hutalisikia tena tuna tunatema mate kulia tufukia kushoto
 
Sijui alikuwa anamaanisha nini ila mimi nimeshaitumia hiyo mbolea.

Najua umeitumia hiyo mbolea, sibishi kwamba mbole ipo au ni nzuri au mbaya.

Nasema, Waziri Mkuu kakazana na maelezo ya malighafi malighafi, malighafi...

Kwa hiyo malighafi inatoka Tanzania malighafi Nairobi?
 
U
Majaliwa ana busara sana, ingekua JPM hapo angemtumbua kwanza boss wa Minjingu phosphate then mengine yafuate.

Hongera Majaliwa kwa kuelewa vema maana ya uongozi..
Unatumbuaje private sector, OK OK OK , unampima kama anakula shisha
 
Back
Top Bottom