Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,806
- 13,574
Salaam Wakuu,
Awali, ikidaiwa kwamba Mwalimu Mkuu (REGIUS MARTIN KAWIMBE Simu Namba *****75299) wa shule ya Msingi Izinga iliyopo kata ya Wampembe, Jimbo la Nkasi Kusini, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa, na ambaye pia alikuwa MSIMAMIZI MSAIDIZI wa uchaguzi katika kijiji cha Izinga, AMEWAFUKUZA SHULE watoto ambao wazazi wao ni wanachama wa CHADEMA kwa madai kwamba ni maelekezo ya wizara ya Elimu yanayosimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu AMBROSE LIJUAKALI.
Soma: DOKEZO - √ - Siasa Zetu: Watoto wa wanachama wa CHADEMA wasimamishwa Shule Nkasi kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na amri ya mwalimu Mkuu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, alipoulizwa na JamiiForums, amesema ameshaona taarifa hii na kuchukua hatua. Kaagiza wadhibiti ubora kwenda kwenye Shule hii kufuatilia jambo hili.
Amesema Wizara inafuatilia kujua ukweli wa taarifa hizi. Haiwezekani Mwalimu ajitungie sheria zake Mwenyewe. Hakuna ubaguzi wowote kwa mtoto wa Mtanzania. Kila mtoto anatakiwa kusoma na Serikali inajenga Shule nyingi sana.
"Kama ni kweli hii taarifa itakuwa ni jambo la ajabu na kusikitisha sana". Amesema Waziri Mienda