Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,629
- 1,206
WAZIRI MHAGAMA AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA WATENDAJI WA CHAMA (CCM) PERAMIHO
Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Peramiho wamehimizwa Kuendelea kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuhakikisha Miradi ya maendeleo inafanikiwa na kutoa huduma sawa sawa kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama Mb) wa Peramiho wakati wa Hafla fupi ya Kukabidhi pikipiki tisa kwa Watendaji wa kata Chama Cha Mapinduzi wa kata ya Peramiho, Maposeni, Ndogosi, Kilagano, Parangu, Kizuka, Litapwasi, Muhukuru, na Mpandangindo iliyofanyika tarehe 08/07/2023 Mkoani Ruvuma.
“Vifaa hivi visaidie kukibeba chama kwanza, katika kusaidia kuongeza idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika maeneo yetu”
Ameongeza kusema Jimbo la Peramiho ni miongoni mwa Majimbo yanayofanya vizuri, katika shughuli za serikali na shughuli za chama.
Aidha, Halmashauri ya Songea imepata hati safi mara mbili Mfululizo, hiyo ni ishara kwamba Uongozi wa chama na uongozi wa serikali wametambua wajibu wao, alisema Waziri Mhagama.