Waziri Mbarawa Punguza punguza parking fee za magari vituo vya SGR

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,010
1,435
Hivi Waziri Mbarawa na Kadogosa hivi kweli wakati mnapanga parking fee ya shilingi 2000 per hour, then 20,000 per one day mli take into consideration ya hali halisi ya maisha ya Mtanzania?

Labda nikwambieni tu kwa mtanzania wa kawaida (Middle Class citizen) ambao ndo wengi na vigari vyao vya mikopo hawawezi kumudu hizo gharama. Mnatesa sana wateja wenu kwa sababu ambazo hazina msingi.

Tunajua mradi umejengwa kwa gharama kubwa lakini sio sahihi kutukosesha amani wasafiri wa SGR kisa parking fee. Gharama za parking fee ni kubwa sana kwa mtu wa kawaida kulipia 20,000 per day.

Mwisho wa siku watu wanaacha magari yao mbali wanapanda boda boda wakipata ajali na kufa hizo treni zinasafiri na ghost client kwani client halisi keshafariki kwa ajali ya boda boda. Hii inatia hasira sana. Shusheni parking fee atleast elfu 3 per day.

Kwa parking fee ya sasa unawaweka wateja wako ambao wengi wao ni watumishi wa umma Dodoma katika risk ya kufa na hizi boda boda wakati angeliweza kuja na gari lake na kuliacha hapo SGR station kwa raha mustarehe na uhakika wa ulinzi.

Sasa hii maegesho ya shilingi 20,000 kwa siku ni mateso kwa wengi. Badilisheni huu utaratibu. Gharama ni kubwa sana hizi wengi hawaziwezi.
 
Back
Top Bottom