Waziri Mavunde: Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji utakaoongeza thamani ya Madini ndani ya Nchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,733
13,493
23d92aaa-58d2-4f43-889a-ab3f3fc56653.jpg
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Tanzania inakaribisha wawekezaji wote wa madini mkakati na kuweka msisitizo kwamba uongezaji thamani wa madin hayo mkakati lazima ufanyike Tanzania.

Mavunde ameyasema hayo leo Bali, Indonesia wakati wa majadiliano juu ya manufaa ya Madini Mkakati katika kukuza uchumi wa nchi wazalishaji ikiwa ni sehemu ya mkutano wa jukwaa la INDONESIA AFRIKA.
1af51af5-1dd1-4941-8035-04019a4f99b1.jpg

08f6d1ae-8787-462d-9545-424c7ff04866.jpg

Waziri Mavunde ameonesha dhamira njema na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia S. Hassan kuvutia uwekezaji nchini na hivyo kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini mkakati ambayo yana mahitaji makubwa Duniani na Tanzania imebarikiwa nayo.

Waziri Mavunde alisisitiza kuwa kwasasa ni sharti la lazima kwamba madini mkakati hayo yaongezwe thamani nchini ili kuvutia viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo betri ya magari ya umeme.

Soma Pia: Waziri Mavunde: Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania Kuwavuta Wawekezaji Duniani Kote
 
Back
Top Bottom