Waziri Masauni: Tutaanza kuhoji wakimbizi kutoka Burundi kwanini wanasita kurejea nyumbani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,806
13,574

WhatsApp Image 2024-06-06 at 18.16.21_db5f3aa9.jpg

WhatsApp Image 2024-06-06 at 18.16.22_3338272e.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mwakilishi wa Serikali ya Burundi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Raia, Theofile Ndarufatiye (kulia), wakibadilishana Nyaraka ya Makubaliano ya Utaratibu wa Urejeaji wa Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa hapa nchini.Tukio hilo imefanyika leo mkoani Kigoma.Jumla ya wakimbizi 158,902 wanahifadhiwa hapa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Serikali ya Tanzania imetangaza kuanza Mpango Maalumu ifikapo mwakani wa kuwahoji Wakimbizi walioko nchini katika Makambi mbalimbali ikiwemo Kambi ya Nduta, Nyarugusu na wanaohifadhiwa katika makazi ya Ulyankulu, Katumba na Mishamo pamoja na vijiji vya mkoa wa Kigoma ambapo jumla ya wakimbizi 158,902 wanahifadhiwa hapa nchini katika kambi za Nyarugusu,Nduta,Makazi ya Ulyankulu,Katumba na Mishamo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kupokea Taarifa ya Kikao cha Wataalamu wa Pande mbili baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Burundi ikionyesha uwepo wa raia wa Burundi wanaogoma kurejea nchini kwao licha ya amani na utulivu kurejea nchini Burundi ambapo pia kabla ya kikao hicho serikali zote mbili zilisaini taarifa ya pamoja ya makubaliano ya urejeaji wa wakimbizi ambapo upande wa Tanzania uliwakilishwa na Waziri Masauni huku upande wa Serikali ya Burundi ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani,Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Raia,Theofile Ndarufatiye.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari,Waziri Masauni aliweka wazi nia ya nchi ya Tanzania kuendelea kuwasaidia nchi jirani zinapokua katika matatizo ikiwemo matatizo ya vita huku akitoa ahadi ya kuendelea kuzisaidia nchi hizo kupokea na kuhifadhi wakimbizi ambao wanakidhi vigezo vya kuwa wakimbizi.

‘Tumefanya vikao mbalimbali na wenzetu kutoka serikali ya Burundi na wametuhakikishia uwepo wa amani na utulivu nchini Burundi lakini kuna baadhi ya wakimbizi wameonyesha nia ya kutotaka kurejea nyumbani na sisi kama serikali tutaendelea kuwaelimisha umuhimu wa kurejea nyumbani na kuungana na wenzao ili kuweza kuliletea maendeleo taifa lao la Burundi,kutokana na hali hiyo ya kusuasua kwa urejeaji wa wakimbizi hao sisi kama serikali tumeona ni vyema mapema mwakani kuwahoji wakimbizi kutoka Burundi kwanini wanasita kurejea nyumbani sambamba na kupima sababu watakazozitoa na kufanya maamuzi sahihi kwa nchi yetu’ alisema Waziri Masauni

Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali ya Burundi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani,Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Raia,Theofile Ndarufatiye alisema serikali ya Burundi inawahakikishi wananchi wake kuwepo kwa amani huku akiishukuru Serikali ya Tanzania kwa wema na ukarimu wa kuwahifadhi rai awa Burundi kipindi chote ambacho kulikuwepo na hali isiyoridhisha ya amani na usalama nchini Burundi.

Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Sudi Mwakibasi alieleza kuwa utaratibu huo wa kuwahoji utazingatia sheria na kanuni zinazosimamia masuala ya wakimbizi duniani huku akiweka wazi kuwa zoezi hilo litaendeshwa kwa mkimbizi mmoja mmoja kuhojiwa na ataethibtika ana haki ya kuendelea kupewa hifadhi ya ukimbizi ataendelea kuwepo kambini na atakaethibitika kutokua na haki hiyo basi atapoteza hadhi ya ukimbizi na atakabidhiwa barua ya kuondoka nchini.
 
Kuwahoji ni kupoteza muda tuu kwakua kwao kumetulia warudishwe kwao warundi ambao wako mitaani kigoma na sahemu zingine Tanzania ni wengi sana kuliko idadi ya walioko makambini wakishazea mji wanajiita waha, wakipuuzwa ipo siku wataingia hadi kwenye nafasi za kimaamuzi
 
Back
Top Bottom