Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,355
- 12,991
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amevitaka Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo kujiandaa na chaguzi zinazokuja ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu (2024) na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani (2025) huku akivitaka vyombo hivyo kuacha milango wazi kwa wananchi wanaofika katika ofisi zao kutoa malalamiko mbalimbali.
Ametoa kauli hiyo mkoani Kilimanjaro wakati akifunga Semina Elekezi kwa Wakuu wa Vyombo vya Usalama,Viongozi Waandamizi na Washiriki wa semina ambapo mada zilizolenga kuwajenga viiongozi hao waandamizi ziliwasilishwa na watoa mada kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
‘Wizara hii ina vyombo ambavyo vimebeba taswira ya Serikali kwa maana nyingine vimebeba taswira ya wananchi,kwahiyo tukiwa tunayatambua hayo na tukitembea na dhana ya 4R tutaenda kuibeba dhana hiyo hasa kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani kwahiyo mjue kwamba wizara hii ni tegemeo kubwa sana na tuhakikishe tunaingia katika uchaguzi nchi yetu ikiendelea kubaki salama," alisema Masauni.
Pia soma: LIVE - Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025