Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 885
Ima kwa kuondolewa na Rais,maamuzi yao au hata Bunge. Hawatabaki. Ni siku itakapotamkwa Mahakamani,Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi,kuwa bomoabomoa haikuwa halali. Zuio la leo ni mwanzo tu.
Zuio la leo haliiachi salama Serikali ya Rais Magufuli. Mchoro wa ubabe na kukurupuka kwa wahusika umeanza kuchorwa. Kesi ya msingi ya Mbunge Mtulia wa Kinondoni itaunguruma. Itatolewa uamuzi. Ili Mawaziri na wahusika wengine wabaki salama,Mahakama ibariki bomoabomoa na kuitupilia mbali kesi ya Mtulia.
Zuio la leo si la kubeza. Ni mwanzo wa mweleka wa kueleweka kwa Serikali ya Rais Magufuli inayoratibu bomoabomoa. Mchezo umeanza!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Zamani ulikuwa mmoja wa vyanzo muhimu hapa JF kuhusu taarifa za ndani za CCM. Then Lowassa akakuharibu kama alivyoharibu mamilioni ya Watanzania wanaoendelea kuota 'mabadiliko hewa.' Hawayataki haya halisi wanayoonyeshwa kwa vitendo na Dkt Magufuli, wanataka yale hewa ya Lowassa.
Hakuna mtu wa kuifunga serikali, afterall, hii si kesi ya jinai. Ilichofanya mahakama ni kutoa zuio tu, si kuharamisha bomoa bomoa. Sote twajua walojenga mabondeni hawana hati stahili. They've just bought some time, lakini soon bomoa bomoa itarudi.
Tujenge nchi, acheni porojo.