Waziri Kijaji: Mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,201
5,586
Mwaka 2023, thamani ya mauzo ya bidhaa kwenda katika Soko la Ulaya iliongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 3.836 kutoka shilingi trilioni 2.446 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 56.8. Ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa za kilimo na viwandani kwenda katika nchi hizo. Aidha, uagizaji wa bidhaa kutoka Jumuiya ya Ulaya ulipungua kwa asilimia 8.1 hadi shilingi trilioni 174.045

mwaka 2023 ikilinganishwa na shilingi trilioni 4.404 kwa mwaka 2022. Upungufu huo ulitokana na kupungua kwa mahitaji ya bidhaa za viwandani na mitaji kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa zilizokuwa zinaagizwa kutoka Soko la Ulaya ikiwemo vilainishi vya magari.

Tanzania iliendelea kuboresha mahusiano ya kibiashara na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Katika kipindi hicho, thamani ya bidhaa zilizouzwa kwenye soko hilo ilikuwa shilingi trilioni 3.022 ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.415 mwaka 2022 ikiwa ni upungufu wa asilimia 16.6 (Jedwali Na. 3).

Hali hiyo imechangiwa na kupungua kwa mauzo ya bidhaa za kilimo, hususan kahawa, chai, mahindi, ngano, mchele, mbogamboga na bidhaa za viwandani zikiwemo vigae, na saruji. Kupungua kwa mauzo, mfano kahawa kumesababishwa na Tanzania kuuza bidhaa husika moja kwa moja kwenye masoko ya nje tofauti na ilivyokuwa awali ambapo bidhaa hiyo iliuzwa kupitia nchi ya Kenya. Vile vile, kuongezeka kwa mahitaji ya ndani kwa bidhaa za ujenzi ikiwemo vigae, saruji, chuma na bidhaa za chuma.

bidhaa zenye thamani ya shilingi trilioni 1.34 ziliagizwa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ikilinganishwa na bidhaa zenye thamani ya shilingi trilioni 1.48 mwaka 2022, sawa na upungufu wa asilimia 9. Upungufu huo umechangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini na kusababisha kupunguza manunuzi ya bidhaa za viwandani kutoka nchi za jirani ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

PIA SOMA:

 
Biashara ilishuka sana tuu Kwa Kanda zote zinazotuzunguka ila ikaongezeka karibu Kwa nusu na Ulaya sijajua Kwa nini japo sababu za Wizara ni ongezeko la mahitaji ya ndani na kupungua Kwa mahitaji ya Nje.
 
Back
Top Bottom