Waziri Jenister Mhagama: Hakuna Serikali ya Magufuli

Siku hizi ukikosea tu, unakuwa jipu na unatumbuliwa papo hapo. Kati ya Magufuli na Mhagama kuna mmoja atakuwa amekosea. Basi watumbuane wenyewe.
 
Je, Kuiita Serikali ya Magufuli ili hali hakuna ruksa ya Mgombea binafsi ni sahihi?

Na hapo hapo kuiita Serikali ya Chama Cha Majipu (CCM), ili hali kuna utumbuaji wa majipu ni sahihi?

Mnaonaje Tukiita Serikali ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Ili huyo Magufuli na Chama Chake Cha Majipu (CCM) wafuate Matakwa ya Wananchi na sio ndoto na Kansa ya Rushwa na Ufisadi inayootesha majipu kila kukicha.
 
CCM ni ile ile. Kama ilivyokuwa, ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa... Kutegemea kuona mabadiliko ndani ya CCM, au mabadiliko nchini kupitia CCM ni ndoto za Alinacha!!!
unadhani mabadiliko yatapatikana kupitia chama gani kwa sasa. tuanzie hapo
 
Huyu Mama nae anataka Kiki kupitia kwenye chama....kwani si ndio huyu aliemkosoa Mwenyekiti kuhusu mkutano mkuu ujao wa kumpa JPM Rungu la chama?

Basi ana kiherehere anatakiwa atoke serikali akapumzike kwenye chama awe wa mipasho! Maana uwajibikaji....naona kama anapwaya sana!! Anajipendekeza kwa JPM nadhani wala sio chaguo la JPM! Mwenzio anataka nshomile na PHD iwepo.....!
 
Yule alikuwa anajisemea tu kwani mkubwa hakosei fuata kanuni hatuna mgombea binafsi. Hayo maneno anatakiwa aseme mgombea binafsi. Watanzania wengi kiswahili shida ndio maana tukitahiniwa kwenye ajira kwenye mashirika yanayohitaji lugha adhimu ya kiswahili tunashindwa na majirani zetu ujanja mdomoni kwa kuiga lafudhi ya kizaramo
 
Marekami wanaseama OBAMA ADMINISTRATION na sio DEMOCRATS ADMINISTRATION.....How about that Miss Mhagama?

key_art_the_obama_administration.jpg
 
Wakati wanakata mauno majukwaani na kujenga umaarufu binafsi badala ya taasisi hawakujua?

Magufuli tumbua mkuu...

Sasa hivi wakisikia jina lako hapakaliki
 
Muda si mrefu tutapata waraka wenye title TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Jina rasmi in Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hayo majina mengine (serikali ya CCM au serikali ya Magufuli) siyo rasmi; yanaonyesha mtawala kwa wakati uliopo)
 
Uchama kwanza anamaanisha magufuli hana nguvu kuizid ccm pale kawekwa na ccm ipo waz hiyo
 
CCM ni ile ile. Kama ilivyokuwa, ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa... Kutegemea kuona mabadiliko ndani yma CCM, au mabadiliko nchini kupitia CCM ni ndoto za Alinacha!!!
mabadiliko yatatokana na chama gani ati?
 
Back
Top Bottom