Mheshimiwa, kwanza hongera yako kuwa muungwana na kusaidia kufikisha hili jambo sehemu husika.Hakika ingekuwa vema sana maana majukumu ya huduma kwa jamii yamegatuliwa kutoka Serikali kuu yakapelekwa waliko wananchi yaani serikali za mitaa yao na vijiji vyao, wakapewa na halmashauri yao na baraza lao madiwani bado na mkuu wa wilaya na vyombo vyote.
Bado ofisi ya mkuu wa mkoa ipo na kuna wizara ya Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa pia.
Sasa huwa ni mtihani mwananchi anatoka huko moja kwa moja wizarani, sijafahamu changamoto ni elimu kuhusu kujua hii mifumo na nguvu zake na wajibu wake au kuna changamoto Gani?
Anyway, pamoja na hayo, mimi kama mtumishi pia, nikiona mtu kaja kwangu nampokea tu namuongoza kwenye utaratibu, mengine hayo baadae. Haya tuendelee kushirikiana.
Hili jambo tayari nimewasilisha ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha tuone wapi tutafika nalo.
Mbarikiwe wote wanaopongeza na kulaumu pia, wote pokeeni baraka za Mungu wa mbinguni 🙏🏽
Nafikili kuna tatizo kwa ngazi za chini. Inaelekea mpaka huyu anawalipotia mtandaoni,ni baada ya kutoona hatua yoyote ikichukuliwa kwa mharifu. Mara nyingi,mtu anatakiwa aende na ushahidi. Polisi au viongozi wengine,kwenye mambo kama haya, huanza kudai mfuta.
Mheshimiwa,hili lenyewe linkatisha tamaa. Kwa hiyo,kuna wakati mtoa mada anaonona tu alichie hivo hivo.
Pia,wapo ambao hawataki ijulikane ndo wametoa taarifa,sababu labda ni majirani au watu wa karibu.
Na uichoke kupokea na kuetea wanyonge na wasio na nguvu,kwanza kukufikilia kwamba unaweza walau ukatoa neno,ni heshima kubwa. Tunajua majukumu ni mengi.
Labda kwa cheo ulichonacho,n wahusika,mungeweka namba ya kutolea taarifa za aina hiyo, ipokee,iombe taarifa zate za mhimu,owasiline na wahusika wa eneo la tukio,lishughulikiwe.
Binafsi naipenda JF,kuna mambo mtaani yanakera,ila,hakuna jambo linaloshindikana likishakuwa humu na kuonekana lina uzito.