Shule ya msingi Kitefu iko Halmashauri ya Wilaya Meru mkoa wa Arusha. Kuna mtoto amefanyiwa ukatili na anadaiwa ni baba yake kwa kumchoma na nyaya za umeme, huyu bwana alikuwepo leo shuleni baada ya kuitwa na Mwalimu Mkuu Mdee.
Kinachokatisha tamaa ni kwamba badala ya huyu bwana kujutia kitendo alichofanya alikuwa akiongea kwa kiburi na dharau kuwa hakuna wa kumfanya lolote kwani hata Polisi wa kituo cha Kikatili hawana uwezo.
Mama wa mtoto ametishwa kuwa akisema ukweli atafukuzwa nyumbani, na siyo mara ya kwanza huyo mtoto kufanyiwa ukatili. Mwalimu mkuu yuko bize na safari za pesa, wiki yote iliyopita alikuwa Dodoma, wiki ijayo atakuwa Morogoro.
Kwa uelewa wangu mhusika na mke wake wangekuwa Polisi sahizi. Cha kusikitisha mwalimu mkuu aliwaambia sihusiki mtajua wenyewe.
Waziri Dkt. Gwajima D hawa ndio watumishi wa Umma, naomba msaidie huyu mtoto, wakamatwe kuanzia baba wa mtoto, mama na mwalimu mkuu kuwa sehemu ya ukatili.
Wahenga wametuambia ukiona tembo amekanyagia mkia wa panya na usipopiga kelele kumsaidia yule panya mkia wake kuachiwa umeshiriki kumkatili yule panya, ndicho alichofanya mwalimu mkuu.