Waziri Bashe acha kuchezea Kodi zetu kwa maono mfu! Kilimo siyo filamu

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,423
55,258
Ni mara ngapi tumeona clip na picha zikionesha wakulima wakilia kwa kukosa masoko ya mazao yao.

*Tushaona nyanya zinauzwa debe sh 500/= na parachichi zikioza huko Iringa.
*Tushaona mahindi yakioza huko Songea na Katavi.
*Tushaona wakulima wa korosho wakiuza korosho kwa bei ya hasara ama kugomea masoko huko Mtwara.
*Tushaona wakulima wakikata mibuni na michai kwa bei mbaya ya mazao hayo.

Kilimo kimeshindwa kuvutia vijana kwasabb 2 tu.
1. Kukosekana kwa masoko ya uhakika ya kumfanya mkulima apate faida (sababu kubwa zaidi hii)
2. Upatikqnaji wa uhakika wa pembejeo na viwatilifu.

Kama wakulima wangekuwa wanapata faida hakuna kijana angekuwa bodaboda, machinga ama mamantilie. Wote wangejikita kwenye kilimo. Shughuli yoyote ya kiuchumi yenye faida huvutia watu.

Kwahiyo siyo kwamba vijana hawataki kilimo kwasbb ya ukosefu wa mitaji....NO.

Nani alitoa mafunzo na mitaji kwa bodaboda, mamantilie na machinga waliozagaa nchi nzima?

Wasomi wa SUA waliomaliza miaka dahali pamoja na maprofesa wao mbana hatuoni wakitumia utaalamu wao kuendesha mashamba makubwa??

Bashe ktk hili unatapanaya tu hela zetu za Kodi lkn zoezi la BBT halitafanikiwa wala halitakuwa endelevu. Kilimo hakiendeshwi hivyo.

Kazi ya serikali kupitia wizara ya kilimo iwe ni kujenga mifumo itakayoifanya shughuli ya kilimo kwenda sawa na kuvutia watu wengi zaidi.

NIMEMALIZA.
 
Bashe is doing for the sake of doing to impress, hii game alishindwa zamani sana..

Hizo hela za block farming angezipeleka kuanzisha na kuendeleza cooperative unions Wakulima wakope pembejeo huko... na serikali idai cooperative unions... sasa hizi blabla ni outdated and we will never go anywhere.
 
Yaani mkulima anateseka huko shambani bei anakuja kupangiwa na dalali ambae hana alichowekeza zaidi ya simu yake mkononi.

Waziri bashe km kweli una nia ya kuwapigania wakulima anza na hawa wanaojiita madalali
Watu walishalalamika sana kuhusu hao madalali lakini wapiii ! Kwa mfano msimu wa maembe pale kiwanda cha azam maembe yataozea kwenye gari usipokubali Dalali anavyotaka !!
 
Huo mradi wao wa BB sijui ni vitu vya ajabu sana. Halafu Samia anasema hataki mchezo. Hivi tumeshajiuliza hii nchi wataalum wa kilimo wanapotelea wapi?

Je kuna wataalamu hasa wa kilimo? Huko SUA wanajifunza nini. Bashe ajifunze juu ya kilimo. Wizara imeshindwa kabisa kuja na majibu. Bashe anachofanya ni kuhakikisha chakula kinapita Kenya kisha kinafika kwao Somalia.

Serikali inapaswa kufanya haya.

1.JKT iwe mfano hasa wa kuhamasisha vijana kujiajiri. Kuwepo na kanda maalamu za kufanya kilimo cha kisasa kupitia JKT mfano Singida ingewekewa mkakaati wa kuja na killimo cha Alizeti na Lindi ikawa na uwezo mkubwa wa kuzalisha Karanga..serikali ingewawezesha vijana kwa kuwakopesha mitaji na kuwatafutia masoko.

2. Drone hizi za Bashe je kuna mafundi wa kutosha na wenye uwezo wa kuziendesha na kuzihudumia? Hapa suluhisho ni kuzifanya VETA na SIDO kuandaa vijana ambao watakuwa na uwezo wa kuzitengeneza. Na sio na VETA na SIDO za 77 na 88 tu.
 
Naunga mkono hoja !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…