Waziri Aweso: DUWASA hakikisha mnatafuta suluhisho la muda mfupi maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji, hasa ya pembezoni mwa Mji wa Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,613
13,294
WAZIRI AWESO ATOA MAAGIZO DUWASA

Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya Kisasa Jijini Dodoma, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa Septemba 05, 2024 katika Kikao Kazi cha Wadau kuhakikisha wanatafuta suluhisho la muda mfupi katika maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa maji,hasa maeneo ya pembezoni.

Mhe. Aweso ametoa maagizo hayo Leo Oktoba Mosi 2024 baada ya wananchi wa maeneo ya Kisasa kulalamikia ukosefu wa maji uliyopo katika maeneo ya Kisasa Bwawani, Kisasa East karibu na relini, Nyumba 300 kuanzia msikitini na Mwangaza.

Mhe. Aweso amesema katika kukabiliana na upungufu wa maji uliyopo katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dodoma inahitajika mipango madhubuti ya muda mfupi ya kuwapatia huduma ya maji wananchi.

Aidha, Waziri Aweso amesisitiza uchimbaji wa kisima kirefu katika eneo la Kisasa ufanyike kwa haraka na Mkandarasi aanze kazi mara moja kabla ya Oktoba 07, 2024 ili wananchi wapate huduma ya maji.

Pia soma;

KERO - Kero ya maji safi jijini Dodoma, Waziri Aweso ingilia kati

IMG-20241001-WA0057.jpg
IMG-20241001-WA0058.jpg
IMG-20241001-WA0059.jpg
IMG-20241001-WA0060.jpg
IMG-20241001-WA0061.jpg
IMG-20241001-WA0062.jpg
IMG-20241001-WA0063.jpg
IMG-20241001-WA0064.jpg
 
Back
Top Bottom