Waziri asema atahakikisha ongezeko la tozo kwenye miamala haliathiri mteja

Hii ramli ya Philip Mpango ya tozo kwenye miamala ya simu haina tofauti na ramli ya uncle Magu ya bei elekezi ya sukari.
 
Kwanini wasitafute vyanzo vingine vya kukata kodi? Yani wanatuvizia kila tukitoa pesa wanajisogeza na kukata tozo,huu si ubinadamu hata kidogo,dawa yao ni kuchonga kibubu cha chuma,nadunduliza mpaka kieleweke.

Kwenye mabenk napo pamekuwa shubiri,mtu umeweka kapesa kako,benki wanaizungusha,ukitoa kiasi wanakata,ukiuliza salio wanakata pesa. Sasa wanataka nini? kwani tozo ndo huko tu zilipo?wajiongeze benki hapajawa salama tena,hizi tozo za kuvizia siyo mpango.
 
Hivi ndugu zangu wa Tz mbona tunakuwa shortsighted kiasi hicho! Serikali imeweka tozo hiyo baada ya makampuni ya simu kuikwepa kabla kwa kutoza chaji kiasi kikubwa kwenye kutuma na siyo kupokea.
Serikali baada ya kugundua janja hiyo(uamuzi wa busara kwa serikali yeyote makini) iliamua kutoza kodi sawa kwenye kutoa na kuweka.
By design, kodi hii inalenga income ya kampuni za simu, na siyo tozo za wateja.
Arguments za kwamba inamlenga mteja wa mwisho hazina mashiko. Sababu hiyo ni sawa na kusema mapato yote ya wafanyabiashara yasitozwe kodi sababu itahamishiwa kwa mwananchi.
Asira zetu tungezielekeza kwa wafanyabiashara wanapohamishia burden ya kodi kwa wananchi, badala ya kuwavimbisha vichwa kufanya uhuni huu
Mkuu angalia post namba 24 halafu tupe kwa kiswahili
 
Kwanini wasitafute vyanzo vingine vya kukata kodi? Yani wanatuvizia kila tukitoa pesa wanajisogeza na kukata tozo,huu si ubinadamu hata kidogo,dawa yao ni kuchonga kibubu cha chuma,nadunduliza mpaka kieleweke.

Kwenye mabenk napo pamekuwa shubiri,mtu umeweka kapesa kako,benki wanaizungusha,ukitoa kiasi wanakata,ukiuliza salio wanakata pesa. Sasa wanataka nini? kwani tozo ndo huko tu zilipo?wajiongeze benki hapajawa salama tena,hizi tozo za kuvizia siyo mpango.

nchi yoyote makampuni ya cm ndio chanzo sahihi cha kukata kodi , hapa kwetu walikuwa unapata mteremko sababu wengi wao walikuwa wanashirikiana NA watumishi wa seikali
 
nchi yoyote makampuni ya cm ndio chanzo sahihi cha kukata kodi , hapa kwetu walikuwa unapata mteremko sababu wengi wao walikuwa wanashirikiana NA watumishi wa seikali
Wamenikosa, mie nimeshakuwa team kibubu
 
RAIS John Magufuli ameagiza kwa taasisi zinazosimamia fedha na kodi, kuhakikisha kuwa serikali inakusanya kodi kwenye miamala ya fedha, inayofanywa na taasisi hizo na kampuni za simu na za madini.

Aidha, ameagiza kuwa Sh bilioni saba zilizolipwa kwa pensheni hewa, zirejeshwe mara moja huku akitoa ufafanuzi wa hatua ya serikali ya kusitisha kwa muda ajira serikalini.

Rais Magufuli alisema hayo Dar es Salaam jana katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na uzinduzi wa sarafu maalumu yenye thamani ya Sh 50,000 na vitabu viwili, kikiwemo vinavyozungumzia masuala ya fedha na uchumi.

Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam, ulikwenda pamoja na kongamano lililojadili mada kuhusu namna ya kupata fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari zake iliyowasilishwa na Profesa Justin Lin wa Chuo Kikuu cha Peiking, China.

Rais Magufuli alisema takwimu zinaonesha katika mwezi mmoja wa Machi, miamala iliyofanywa na kampuni za simu za mkononi ni ya zaidi ya Sh trilioni 5.5, lakini alihoji ni kasi gani cha kodi kimeingia serikalini.

Alisema pamoja na kusimamia makusanyo ya kodi za serikali, pia aliagiza BoT, Hazina na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wajipange kuhakikisha mtambo wa kudhibiti makusanyo ya kodi, unafanya kazi na kufuatilia usalama wa huduma za fedha.

Mbali na hilo, aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha serikali inakusanya kodi zinazostahili kutoka kwenye kampuni za madini na kufuatilia kwa karibu, kwa kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya kampuni.

“Unakuta kampuni ipo nchini mwaka wa kwanza hadi wa 10, wanakwambia hawapati faida lakini wanaendelea kuchimba dhahabu. Sasa eneo hilo liangaliwe kwa karibu na kama kampuni inashindwa bora iondoke, ni heri tubaki na dhahabu yetu hata miaka 1000 ijayo, watakuja kuchimba wengine wakati sisi tumeshaoza. Visingizio vya kupata hasara kila mwaka, lakini wanaendelea kuwepo, haiwezekani,” alisema.
 
Mabenki yashatoa matangazo ya kuongeza gharama kwa sababu ya ongezeko la kodi.

Waziri halijui hilo?
 




Waziri wa fedha Dk. Philip Mpango amesema watakuwa wanawabana makampuni ya simu ili wasije wakawaumiza wateja kwa tozo kubwa kutokana na ongezeko la kodi walilofanya kwenye bajeti hii na ushuru waliouweka sasa hivi utalipwa na kampuni ya simu na mabenki na sio mtumiaji wa huduma hilo litakaguliwa na TCRA, TRA na BOT

Ishu ya analogue ya Sukari iliwashinda itakuwa hii ya kidigitali???
 
yupo wapi waziri?

Kila mwenye akaunti benki atakuwa ameshapata ujumbe huu hadi sasa

Ndugu mteja, tunapenda kukufahamisha ongezeko la 18% kama VAT katika gharama zote za kibenki kuanzia 01.07.2016 kama ilivyoainishwa kwenye bajeti ya 2016/2017
 
!
!
Mbombo itolo nkamugwango
 

Attachments

  • IMG-20160701-WA0007.jpg
    IMG-20160701-WA0007.jpg
    45.7 KB · Views: 27
Huyu jamaa muongo mm leo nimetoa pesa wamekata ile asilimia yao....
 
"Nawashukuru sana wa-Tz nawaahidi kua SITAWAANGUSHA"-nimeshau msemaji alikua nani.
 
Back
Top Bottom