Wazee wa CUF Temeke watoa tamko juu ya Prof. Lipumba kurudi katika uongozi CUF

Dah, hivi kwel mfano mtu unaweza jiuzulu (resign kazi) kisa hukufurahishwa na mambo yanavyoenda ndani ya hiyo organization /company, kesho ukarudi ukasema unatengua kauli /tengua barua? urudishwe kazini, huu ni zaidi ya "uhuni"

Prof. Lipumba hastahili hats kugombea nafasi hiyo na mwenyekiti mtarajiwa....anafanya njama na anataka kukiharibu chama, alianza Hamadi akashindwa na sasa ni Prof, nae atashindwa, CUF kuweni Makini, you are at the very best in the interest of this nation, prof aliwaacha kipindi mnamhitaji Sana, it may take another waste of 10years to get rid of him, with the same style.
 
ninaamini katika wakati,wakati wenyewe utaongea katika hili na wengi watabaki vinywa wazi,wakisema "imekuwaje"?????????
 
Washakusanywa hao na kupewa chochote UKAWA inawasumbua ,watahonga sana kuwavuruga UKAWA lakini ushetani wao utafeli.
Haya ni mambo ya CUF kina ngangali ukawa wanaingiaje hapa. Tena wazee wazee wamesema hakuna kifungu kilichokiukwa lipumba kutengua barua yake ya awali, tatizo lipo wapi?
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Washakusanywa hao na kupewa chochote UKAWA inawasumbua ,watahonga sana kuwavuruga UKAWA lakini ushetani wao utafeli.
hahahah ushetani kamanda uliletwa na group la watuhumiwa waliohamia ukawa kuja kutafuta vyeo, kiasi cha kuwafanya viongozi waadilifu hawa kutimkia wanapopajua wao. ni uharamia wa ajabu sana hatutasahau hii kitu. tuliambiwa inabidi tubadilishie gia angani.
 
Hawa Kwani Si Ndiyo Wale wale Wanaojiita Wazee wa Timu ikisha Wakazikoroga Yanga na Simba?
 
Wanasubiri tu mwezi wa ramadhan upite ,moto utakao waka pale CUF kila kibaraka wa UKAWA genji ndani ya CUF atafunga domo lake
 
Tamko la jumuiya ya wazee CUF-Wilaya ya Temeke juu ya Prof. Lipumba kurudi katika uongozi.

Mnamo 17/06/2016 kamati ya uogozi ya cuf taifa ilitoa tamko, iliyo ipa kichwa cha habari “kauli tata ya Prof. Lipumba kuhusu kurudi ktk nafasi yake ya uenyekiti wa taifa” baada ya kuipitia taarifa hiyo kwa kina, tumebaini kuwa kamati ya uongozi ina lengo la kumchafua Prof. Lipumba, katika jamii na kwa wana cuf kwa ujumla, kwa kudai Prof. Lipumba anakigawa chama, jambo ambalo sio kweli.

Prof. Ibrahim Lipumba, kamuandikia barua Katibu Mkuu wetu juu ya kuifuta barua yake ya kujiuzuru, ni jambo zuri, jambo hili la kuandika barua ya kufuta barua yake ya kujiuzuru linakigawa vipi chama?

Lini kikao cha baraza kuu, kilikaa na kikabaini kuwa barua ya Prof. Lipumba ya kufuta barua ya kujiuzuru ni tata, na inalengo ya kukigawa chama?

Sisi kama wazee tunahoji , yale maswali kadhaa ambayo yameulizwa katika hilo tamko la kamati ya uongozi, lini walimwita Prof. Lipumba katika kikao chao chochote ili wamuulize halafu Prof. Lipumba, hakutokea?

Je, wanataka Prof. Lipumba, na yeye aite vyombo vya habari ajibu? Hii busara ya kamati ya uongozi ni ya ajabu sana, na sisi tunaona ndio inakigawa chama.

Sisi hatuungi mkono prof lipumba kuita vyombo vya habari kujibu lolote kwa sasa, na pia tunaliona tamko la kamati yauongozi ni la kukurupuka sana, lenye lengo moja tu kumvunjia heshima Prof. Lipumba, tunalaani sana sana suala hilo.

Prof. Lipumba ni mtu muhimu ktk chama chetu, kama wazee hatuwezi tukavumilia jambo lolote la kihuni la kumvunjia heshima kiongozi huyu lifanikiwe.

Kutokana na ushauri tuliopewa na wanasheria, tumebaini hakuna utata wowote, iwe wa kisheria au kikatiba kwa kingozi aliyejiuzuru ktk chama chetu kuomba kurudi ktk uongozi.

Tunataka vikao halali vya chama ndio vijadili na kuamua, suala hili. Na maswali yenu yote kadhaa mumulize katika vikao na tunaamini atawajibu na mtamuelewa tu.

Mungu ibariki CUF, Mungu ibariki Tanzania.

Mzee Bakari Juma Mtanga
M/kiti Jumuiya ya Wazee Wilaya ya Temeke.
20/06/2016
Namshauri lipumba hizo noti anazo zipoteza azitunze kusudi zimsaidie baadae maishani maana huo uenyekiti ndio au sahau
 
Back
Top Bottom