Wazee wa CUF Temeke watoa tamko juu ya Prof. Lipumba kurudi katika uongozi CUF

s.massaun

Member
Dec 20, 2010
82
12
Tamko la jumuiya ya wazee CUF-Wilaya ya Temeke juu ya Prof. Lipumba kurudi katika uongozi.

Mnamo 17/06/2016 kamati ya uogozi ya CUF taifa ilitoa tamko, iliyo ipa kichwa cha habari “kauli tata ya Prof. Lipumba kuhusu kurudi ktk nafasi yake ya uenyekiti wa taifa” baada ya kuipitia taarifa hiyo kwa kina, tumebaini kuwa kamati ya uongozi ina lengo la kumchafua Prof. Lipumba, katika jamii na kwa wana CUF kwa ujumla, kwa kudai Prof. Lipumba anakigawa chama, jambo ambalo sio kweli.

Prof. Ibrahim Lipumba, kamuandikia barua Katibu Mkuu wetu juu ya kuifuta barua yake ya kujiuzuru, ni jambo zuri, jambo hili la kuandika barua ya kufuta barua yake ya kujiuzuru linakigawa vipi chama?

Lini kikao cha baraza kuu, kilikaa na kikabaini kuwa barua ya Prof. Lipumba ya kufuta barua ya kujiuzuru ni tata, na inalengo ya kukigawa chama?

Sisi kama wazee tunahoji , yale maswali kadhaa ambayo yameulizwa katika hilo tamko la kamati ya uongozi, lini walimwita Prof. Lipumba katika kikao chao chochote ili wamuulize halafu Prof. Lipumba, hakutokea?

Je, wanataka Prof. Lipumba, na yeye aite vyombo vya habari ajibu? Hii busara ya kamati ya uongozi ni ya ajabu sana, na sisi tunaona ndio inakigawa chama.

Sisi hatuungi mkono prof lipumba kuita vyombo vya habari kujibu lolote kwa sasa, na pia tunaliona tamko la kamati yauongozi ni la kukurupuka sana, lenye lengo moja tu kumvunjia heshima Prof. Lipumba, tunalaani sana sana suala hilo.

Prof. Lipumba ni mtu muhimu ktk chama chetu, kama wazee hatuwezi tukavumilia jambo lolote la kihuni la kumvunjia heshima kiongozi huyu lifanikiwe.

Kutokana na ushauri tuliopewa na wanasheria, tumebaini hakuna utata wowote, iwe wa kisheria au kikatiba kwa kingozi aliyejiuzuru ktk chama chetu kuomba kurudi ktk uongozi.

Tunataka vikao halali vya chama ndio vijadili na kuamua, suala hili. Na maswali yenu yote kadhaa mumulize katika vikao na tunaamini atawajibu na mtamuelewa tu.

Mungu ibariki CUF, Mungu ibariki Tanzania.

Mzee Bakari Juma Mtanga
M/kiti Jumuiya ya Wazee Wilaya ya Temeke.
20/06/2016
 
wanaCHADEMA ndio wanaopinga Lipumba kurudi CUF. wengi wao wanamchochea Mtatiro awashawishi viongozi wa CUF kumtosa Lipumba.
WanaCUF wenyewe bado wana imani na Lipumba pamoja na kumpinga kwake Lowassa.
 
Toka CUF iasisiwe ndio leo kwa mara ya kwanza ninasoma kuwa kuna wazee wa CUF

Wazee wa siku hizi wanatia shaka sana
Hawa watakuwa wale wazee wa Dar es Salaam wa JK
Mtu kajiuzulu kwa hiari yake mwenyewe baada ya kutoridhishwa na mambo ndani ya chama. Anarudi baada ya mwaka mmoja na kudai nafasi yake kwa uataratibu upi? Huu ni upuuzi. na hao wazee ngoja niishie hapa tu nisije nikaitwa mkosa adabu.
 
Naona Prof. anajaribu kivingine. Ni upepo tu. CUF wamepitia mitihani migumu zaidi ya huu.
 
wanaCHADEMA ndio wanaopinga Lipumba kurudi CUF. wengi wao wanamchochea Mtatiro awashawishi viongozi wa CUF kumtosa Lipumba.
WanaCUF wenyewe bado wana imani na Lipumba pamoja na kumpinga kwake Lowassa.
Of course CHADEMA wana maslahi na CUF ndani ya UKAWA. huyu Lipumba si amewatosa wakati ndipo alikuwa anahitajika zaidi? kimebadilika nini hadi sasa aone CUF imekuwa paradiso?
 
wanaCHADEMA ndio wanaopinga Lipumba kurudi CUF. wengi wao wanamchochea Mtatiro awashawishi viongozi wa CUF kumtosa Lipumba.
WanaCUF wenyewe bado wana imani na Lipumba pamoja na kumpinga kwake Lowassa.
Ata ubongo wako unajuwa kuwa wanachadema wana akili sana sema kwa sababu wewe ni wa chama cha kijani ndio maana bado unakula pumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…