SoC03 "Wazee wa cha juu" : Jinsi udalali unavyoua soko la ndani

Stories of Change - 2023 Competition
Aug 14, 2016
7
6
Maisha ya kawaida ya mtanzania ni pamoja na uwakala wa bidhaa na huduma au maarufu kama ujulikanavyo "udalali".

Tangu kupanda kwa jua mpaka machweo yake, watu wanatafuta masoko ya bidhaa zao ama fursa mpya --waitavyo wenyewe "chimbo" .

Lakini mimi binafsi bwana kuna jambo moja linalonikera sana kwenye mtindo huu wa utafutaji riziki

KERO

Mbali na kurahisisha upatikanaji wa huduma husika, changamoto kubwa ya udalali ni "zusho/ongezeko kubwa la bei" lililozoeleka kama "cha juu" Yaani hawa ndugu zetu wamekuwa hodari katika kuongeza na kuutanua "mnyororo wa thamani"/(value chain) kwa misuko isiyo lazima, jambo linalopelekea bei za bidhaa ama huduma husika kuwa juu kupita kiasi. Hii huchelewesha sana upatikanaji wa bidhaa au huduma hiyo kwa wakati na gharama stahiki.

Tuikemeeee...!🗣️🗣️🗣️

Haijalishi ni pango la nyumba ama ofisi, mauzo ya viwanja ama mashamba na mifugo, usafiri na vyombo vyake, kama stendi za mabasi ya mikoani, utitiri wa madalali katika kila pembe ya uchumi wetu ni kerooo, tuikemee.

CHANZO
Sijui huko zamani sana hali ilikuwaje, lakini binafsi ninauhusisha huu wingi wa madalali katika siku za hivi kar ibuni ndani ya nchi yetu na mambo kama;- Mosi, kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu huku shughuli za kiuchumi kwa sehemu kubwa zikiwa zimebaki ni zile zile

Pili, ni idadi kubwa ya wahitimu wa shule za kati na vyuo ambao wamelizidi uwezo soko la ajira na hivyo kuzagaa kwa vijana wengi wasio na ajira thabiti za kukimu mahitaji yao na matarajio ya familia zao.

Aidha, uhamiaji holea wa watu na uhodhi bidhaa ambao kwa kiasi kikubwa husababisha wimbi kubwa kujiingiza katika janja janja za mauzo al-maarufu kama udalali

MWAROBAINI

Rashid mie, katika tafiti na tafakuri zangu za namna gani ya kutafuta suluhu ya kero hii, nimekusanya kikapu cha yafuatayo kama mambo ya awali ya kufanyika nchini kwetu

Urasimu na upangaji viwango wa kazi za kidalali
Watu wa mauzo ni sehemu ya msingi mno kwenye ulimwengu wa biashara, kwani kama neno lenyewe ""dalali"" au "dalili" linavyo maanisha kwa kiarabu..muonesha/kiashiria. Ni lazima wateja waonyeshwe lakini kiwanda hiki kikirasimiwa na kuwekewa utaratibu upo uwezekano mkubwa wa kutunza na kuliimarisha soko letu la ndani la bidhaa.

Matumizi ya 'TEHAMA' katika utangazaji, na uuzaji bidhaa na huduma.
Karne ya 21 ina bahati ya kipekee ya urahisi wa kimawasiliano baina ya taasisi na watu binafsi. Haya yapigiwe debe yatumike na idara zote nyeti za masoko ili ma dalali wa kati wengi wapunguzwe, jambo litakalosaidia kupunguza mnyororo wa thamani na hivyo kutuliza mwenendo wa soko.

Vyombo vya kisheria na kijamii vinavyoshughulikia kesi za mdalali
Mimi naona ipo kabisa haja ya kuwepo kwa sheria husika na vyombo vya nguvu vya kudhibiti hawa jamaa, maana kuna muda hujiingiza kwenye utapeli na wizii holela wa mali za wateja. Uwepo wa vyombo hivi vya kijamii pia utasaidia kutatua migogoro mingine ya kidalali kama malipo ya kodi ya mwezi mmoja eti kwa pango.

Halafu kutoa elimu na hamasa ya utafutaji kwa vijana
unajua endapo hawa vijana watafundishwa na kupewa mapema hamasa za kujiajiri na kutia moyoni kwamba jamii yao inayategemea wao kuunda vyanzo vipya vya ajira kama viwanda, hawataamka usingizi wa kusubiri ajira na hivyo muitiko wa udalali litabaki kuwa chaka la wengi kufugia uvivu wao. Kwa hiyo elimu na mikopo wezeshi ya mitaji itolewe ili kero hii ipungue

Ni kweli kabisa kwa nchi zinazoendelea kama hii ya kwetu, Tanzania, ajira zimekuwa finyu, ila huu sio mlango wa vijana wengi kuulea utamaduni nduli(adui) wa "uvivu" kwa kijiingiza bila msingi katika huu ubwanyenye wa udalali. Na vile vile kwa zama hizi, wakati tukiyaelekea kwa kasi maendeleo ya viwanda nchini mwetu ni muhimu sana sana, kwa madalali ambao tayari wako katika fani kujifunza na mambo mengine ya kuwaongezea kipato kama ujasiriamali na ujasiriahuduma ili waweze kudalalia huduma zao wenyewe kwa bei rahisi na elekezi yenye kumlinda mtanzania wa kawaida na soko lake la ndani. Ahsanteni wana JF

Rashid Athumani
 
Udalali utaendelea kuwepo, maana changamoto ya vatu wengi zaidi ni mitaji. Lakin zikuwekwa taratibu nzuri jambo hili litampunguzia sana mwananchi usumbufu
 
Kwa namna yoyote ile udalali hauwezi kuisha kwa sababu chache na laini kabisa.

1. Sio wenye mali wote wanajua masoko husika na watu husika wanaoweza kuwa wateja wao.

2. Shida za dunia husababisha watu kutafuta mnunuzi wa mali zao kwa haraka ( saa zingine madlali hununua, iwe mazao, magari, nyumba n.k) ili kulinda na kustahimili madeni na shida walizonazo.

3.uhitaji wa "platform" stahiki kwa kile kinachouzwa iwe real estate, vifaa vya ndani au magari. Unaweza post popote pale mali yako na isiuzike kwa muda stahiki kwako wa kutimiza malengo. Hapo ndipo madalali huingia. Wacha nikuoe mfano:

Una shida na unataka kuuza kiwanja au nyumba yako.umeipost au umeelezea ndugu zako na wameshindwa kukunasua. Hivyo unam consult dalali apambane kupata mnunuzi (kumbuka hawa watu wana connection/ wanarahisisha maisha) yule dalali anakua amesajiliwa rasmi na ana vibali vyote, mkiandikishana hata atokee ndugu yako ananunua lazima utoe commission kwake na kampuni yake. Hivyo mnunuzi na muuzaji kikawaida hamuwezi kukutana (labda itokee) pasipo dalali

Katika mali chache nlizowahi kunujua na dalali akiwepo nimegundua ukishajua vommission anayotaka ni rahisi kupata bei halisi ya mali unayotaka iwe nyumba, chombo au gari. Hii haihusiani na mikoa yenye utapeli mwingi ambayo hata mwenye mali huwezi kutana nae (mnaijua)

4. Patana vommission kabla ya kuongea biashara. Hii itakusaidia kuondokana na maumivu (psychological) katika hela anayopatiwa yeye dalali. Mfano umependa nyumba ya milioni 40, dalali anataka milioni 2. Wewe inakuwia ugumu gani kuomba upunguziwe hadi 30 na ukampa dalali 2M ili ubakiwe na 8M ? Saa zingine ni uvivu wa kufikiria unatukosti. Sasa ukute ntu anauza nyumba 35M unambembeleza (baada ya kukutanishwa) hadi 25M anakwambia natoa 1M na wewe utoe 1M kwa dalali ila roho yako inakuuma wakayi hakuna namna ungekutana na huyu mtu pasipo dalali kuifikisha kwenye platform unaiona wewe na kuvutiwa nyo? Huu pia ni lowkey uchawi
 
Kweli kabisa kamanda udalali lazima hata iweje bile....hata hivyo.mimi kwenye makala hii niliangazia zaidi swala la jitihada za urasimishaji katika sekta hii..Kwamba kama jamii .kuwe kuna miongozo maalum inayo simamia harakati za udalali ili...suala la ununuzi na uuzaji visiwe kero wala chaka la matapeli na wavivu...

Shimo pana lililopo kwenye mazingira ya ufanyaji wake kwa sasa lime utia wengi wasiopenda kazi kupaona kama sehemu ya kupigia hela za urahisi..

Siku hizi kwa mfano kuna agents za kudalali zipo mitandaoni kwa huduma mbali mbali...huduma zibaakisi kabisa usasa na hata malipo yanaakisi kabisa dhima anayoicheza dalali katika kufanikisha zoezi zima la biashara (mbadilishano)

Shukran kwa mchango
 
Maisha ya kawaida ya mtanzania ni pamoja na uwakala wa bidhaa na huduma au maarufu kama ujulikanavyo "udalali".

Tangu kupanda kwa jua mpaka machweo yake, watu wanatafuta masoko ya bidhaa zao ama fursa mpya --waitavyo wenyewe "chimbo" .

Lakini mimi binafsi bwana kuna jambo moja linalonikera sana kwenye mtindo huu wa utafutaji riziki

KERO

Mbali na kurahisisha upatikanaji wa huduma husika, changamoto kubwa ya udalali ni "zusho/ongezeko kubwa la bei" lililozoeleka kama "cha juu" Yaani hawa ndugu zetu wamekuwa hodari katika kuongeza na kuutanua "mnyororo wa thamani"/(value chain) kwa misuko isiyo lazima, jambo linalopelekea bei za bidhaa ama huduma husika kuwa juu kupita kiasi. Hii huchelewesha sana upatikanaji wa bidhaa au huduma hiyo kwa wakati na gharama stahiki.

Tuikemeeee...!

Haijalishi ni pango la nyumba ama ofisi, mauzo ya viwanja ama mashamba na mifugo, usafiri na vyombo vyake, kama stendi za mabasi ya mikoani, utitiri wa madalali katika kila pembe ya uchumi wetu ni kerooo, tuikemee.

CHANZO
Sijui huko zamani sana hali ilikuwaje, lakini binafsi ninauhusisha huu wingi wa madalali katika siku za hivi kar ibuni ndani ya nchi yetu na mambo kama;- Mosi, kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu huku shughuli za kiuchumi kwa sehemu kubwa zikiwa zimebaki ni zile zile

Pili, ni idadi kubwa ya wahitimu wa shule za kati na vyuo ambao wamelizidi uwezo soko la ajira na hivyo kuzagaa kwa vijana wengi wasio na ajira thabiti za kukimu mahitaji yao na matarajio ya familia zao.

Aidha, uhamiaji holea wa watu na uhodhi bidhaa ambao kwa kiasi kikubwa husababisha wimbi kubwa kujiingiza katika janja janja za mauzo al-maarufu kama udalali

MWAROBAINI

Rashid mie, katika tafiti na tafakuri zangu za namna gani ya kutafuta suluhu ya kero hii, nimekusanya kikapu cha yafuatayo kama mambo ya awali ya kufanyika nchini kwetu

Urasimu na upangaji viwango wa kazi za kidalali
Watu wa mauzo ni sehemu ya msingi mno kwenye ulimwengu wa biashara, kwani kama neno lenyewe ""dalali"" au "dalili" linavyo maanisha kwa kiarabu..muonesha/kiashiria. Ni lazima wateja waonyeshwe lakini kiwanda hiki kikirasimiwa na kuwekewa utaratibu upo uwezekano mkubwa wa kutunza na kuliimarisha soko letu la ndani la bidhaa.

Matumizi ya 'TEHAMA' katika utangazaji, na uuzaji bidhaa na huduma.
Karne ya 21 ina bahati ya kipekee ya urahisi wa kimawasiliano baina ya taasisi na watu binafsi. Haya yapigiwe debe yatumike na idara zote nyeti za masoko ili ma dalali wa kati wengi wapunguzwe, jambo litakalosaidia kupunguza mnyororo wa thamani na hivyo kutuliza mwenendo wa soko.

Vyombo vya kisheria na kijamii vinavyoshughulikia kesi za mdalali
Mimi naona ipo kabisa haja ya kuwepo kwa sheria husika na vyombo vya nguvu vya kudhibiti hawa jamaa, maana kuna muda hujiingiza kwenye utapeli na wizii holela wa mali za wateja. Uwepo wa vyombo hivi vya kijamii pia utasaidia kutatua migogoro mingine ya kidalali kama malipo ya kodi ya mwezi mmoja eti kwa pango.

Halafu kutoa elimu na hamasa ya utafutaji kwa vijana
unajua endapo hawa vijana watafundishwa na kupewa mapema hamasa za kujiajiri na kutia moyoni kwamba jamii yao inayategemea wao kuunda vyanzo vipya vya ajira kama viwanda, hawataamka usingizi wa kusubiri ajira na hivyo muitiko wa udalali litabaki kuwa chaka la wengi kufugia uvivu wao. Kwa hiyo elimu na mikopo wezeshi ya mitaji itolewe ili kero hii ipungue

Ni kweli kabisa kwa nchi zinazoendelea kama hii ya kwetu, Tanzania, ajira zimekuwa finyu, ila huu sio mlango wa vijana wengi kuulea utamaduni nduli(adui) wa "uvivu" kwa kijiingiza bila msingi katika huu ubwanyenye wa udalali. Na vile vile kwa zama hizi, wakati tukiyaelekea kwa kasi maendeleo ya viwanda nchini mwetu ni muhimu sana sana, kwa madalali ambao tayari wako katika fani kujifunza na mambo mengine ya kuwaongezea kipato kama ujasiriamali na ujasiriahuduma ili waweze kudalalia huduma zao wenyewe kwa bei rahisi na elekezi yenye kumlinda mtanzania wa kawaida na soko lake la ndani. Ahsanteni wana JF

Rashid Athumani
MPYA HII,hapa mfanyabiashara na mtumiaji wa viazi mviringo,,,,,,,,,,(kiepe)
Msimu umewadia.tenaaaaaa,
KARIBU,mkoa wa
NJOMBE,kusini mwa Tanzania, ujipatie viazi mviringo aina zote,unazotaka wew kwa bei nafuu,kabs,....
Wewe dalali na mfanyabiashara mnakaribishwa,....
bei maelewano,
Mawasiliano 0620743697.
 
Back
Top Bottom