Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 228
- 268
Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa ya Takwimu (NBS) kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 inaonyesha Mkoa wa Tabora unaongoza kwa watu wake kutokujua kusoma na kuandika jambo linalosababisha wengi wao kukosa haki zao za msingi kutokana na changamoto hiyo.
Uchunguzi wangu umebaini Watoto wa kike na wale wa kiume wenye umri wa Miaka 8 - 15 wanaongoza kuwa watumwa (kupewa ajira katika umri mdogo) jambo linalochangia kwa kiwango kikubwa anguko la mkoa huo kuwa na wasiojua kusoma na kuandika kwa kiwango kikubwa.
Sababu kubwa ya ongezeko la wasiojua kusoma na kuandika linasababishwa na baadhi ya wazazi kutokuwa na fedha za kuwahudumia gharama kadhaa za shule, hivyo hulazimika kuwatumikisha, mfano kwenye minada na magulio kufanya biashara za familia na wakati mwingine kuajiriwa na wale wenye mizigo mikubwa ili waweze kupata fedha za kujikimu kimaisha.
Walichosema Wazazi
Masumbuko Elia, Mkazi wa Sikonge alisema analazimika kuwatuma watoto wake wakafanye kazi ya kuuza mazao na kuku kwenye minada ili familia ipate chakula na fedha za matumizi mengine kwakua hawaendi shule.
“Mimi ninao watoto watatu ambapo wote hawajafanikiwa kwenda shule, changamoto kubwa ni pesa za kuwalipia mahitaji yao, naona ni rahisi kuwatuma Mnadani kuuza kuku na nafaka za hapa nyumbani ili walete pesa hapa na wameshazoea kabisa, wanatusaidia kwa kiasi kikubwa sisi kama Familia na sitamani kabisa waende shule” alisema alisema na kuongeza:
“kuhusu Elimu, mimi kwetu sijasoma kwahiyo naona hakuna umuhimu wa wao kwenda shule, ndiyo maana naamua kuwafundisha kazi za kujikimu maisha katika umri mdogo ili wakikua wasinisumbue lakini hata serikali inaweka mkazo waende kusoma lakini mimi sina fedha za kuwasomesha kabisa.”
Mzazi mwingine mkazi wa Tabora Manispaa aliyejitambulisha kwa jina la Idrisa Said alisema yeye anawatuma watoto wake mara mbili kwa wiki kwenda kwenye magulio na haoni hasara kwao kwani shule wanaenda lakini wanakosa masomo mara moja kwa wiki.
“Mimi kwa sasa umri wangu ni mkubwa na mke wangu alifariki, sasa kwa sasa sina msaidizi kwahiyo hawa watoto waliobaki ndio wananisaidia kutafuta fedha za kujikimu mahitaji nyumbani, huwa nawatuma kwenda kuuza maharagwe sokoni kwa kutumia baiskeli na wanaenda mnadani siku ya jumatano na jumapili na wanaleta pesa ambayo inaisaidia familia kwenye vitu vidogo vidogo” alisema mzazi huyo.
Wanachosema Watoto
Mtoto mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abas Hassan 11, Mkazi wa Ipuli Manispaa ya Tabora anasema yeye ameacha kwenda shule akiwa darasa la pili na akalazimika kuanza kumsaidia mama yake kuuza bidhaa mbalimbali ili ajipatie kipato.
Anasema “Tumezaliwa wanne nyumbani na mimi ndio wa kwanza nyumbani kwetu lakini wakati tukiendelea na maisha Baba akakimbia, tukabaki na Mama sasa nyumbani familia ni kubwa, kwahiyo mama akaanzisha mradi wa kuuza Viazi sokoni na mayai ya kuchemsha, awali nilikuwa naenda naye ila siku hizi naenda mwenyewe na kazi hii naifanya mara tatu kwa wiki kwahiyo sipati muda kabisa wa kwenda shule.
“Kwa umri wangu wa miaka 11 nilitakiwa kuwa darasa la nne ila siwezi kusoma tena lakini bado nahitaji kwenda kusoma nikipata wa kunisimamia naweza kwenda kusoma maana inaniuma wenzangu wako shule mimi nahangaika na kuuza bidhaa sokoni.”
Iko wazi kwamba wazazi wamekuwa wakiwafanyia ukatili watoto wao bila kujua tena muda ambao watoto wenzao wako darasani na wakati mwingine watoto hawa wanafanya kazi hadi wanatembea usiku huu ni ukatili mkubwa ambao wanaufanya wazazi na walezi waliowengi.
Hata hivyo, changamoto kubwa iliyopo kwa wazazi na walezi wa Tabora ni kwamba wanaona ukatili kama jambo la kawaida na hata linapofichuliwa hawapo tayari kutoa ushirikiano jambo linalosababisha kesi nyingi kufutwa mahakamani kwa ukatili unaokuwa umetendeka kwa watoto.
Jitihada za Serikali kuwasaidia kielimu
Hivi karibuni kupitia kwa mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Hamis Mkanachi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo ulitangaza mkakati wa kuwarejesha watoto wote ambao wako nje ya mfumo wa elimu ili waweze kupata elimu kama watoto wengine.
Mkanachi alisema kwa Mwaka 2024 zaidi ya watoto walioandikishwa kuanza madarasa ya awali na shule za msingi wapatao 27114 sawa na asilimia 33.1 hawapo shuleni na watoto wa kiume kati ya hao ni 15930 huku watoto wa kike wakiwa ni 11183.
Mkanachi aliendelea kusema kwamba serikali imedhamiria kuwarejesha shuleni watoto wote ambao waliacha masomo kwa sababu ambazo hazijulikani lengo ikiwa ni kuondoa kizazi cha wasiojua kusoma na kuandika katika mkoa huo ambapo serikali itagharamia mahitaji yote muhimu kwa watoto hao.
Waraka wa Elimu namba 2 wa mwaka 2021 unaeleza ya kuwa dira ya taifa ni kuwa na watanzania wenye maarifa, ustadi, umahiri na uwezo wa mitizamo chanya kwa watu wake pia mwongozo huo unaelekeza namna wanafunzi ambao hawako shule wanavyoweza kusoma tena na kutimiza ndoto zao.
Hivyo wazazi, walezi na wadau wengine wasiruhusu watoto wao kutumikishwa badala ya kupewa elimu itakayomsaidia mtoto kwenye maisha ya baadae, kwani vitendo vya watoto kuacha masomo na kujikita kwenye biashara wakati wako kwenye umri wa masomo sio sahihi na halikubaliki, likiendekezwa tutazalisha taifa la wajinga na wapumbavu ambao hawaelewi lolote na hapo ndipo mdororo utakapoanzia.
Kwenu wanajamvi.