Watumishi wa UDART wagoma wakidai malipo na mkataba

Hivi kwanini nchi hii inapenda migogoro isiyokuwa na sababu.!? watu hata mwaka bado tayari washaanza malalamiko.!

Tuko nyuma jamani tujitambue
Mkuu nadhan wewe hujawai kufanya kazi ya kulipwa mshahara mwisho wa mwezi.. Pia kuna uwezekano bado unalishwa na wazazi..

Mwenzako hajalipwa mshahara miez miwili na bado unataka aendelee kuhenya, mtu hana mkataba wa kazi we unataka aendelee kupigika kama mjinga tu
Walichofanya ni haki na ni sahihi hata kisheria.
Kuwa na roho ya imani ndugu...
 
Na mshahara wanaanza kupokea tangu kipindi gani baada ya kuanza kazi? Au wasubiri kampuni ipate faida?
 
Walipwe halafu wafukuzwe na waajiriwe wengine haiwezekani wagome wakati mradi bado mchanga na wao bado hawajaaminiwa kwenye kazi
Mkuu,kama hawajaaminiwa ndo wasipewe kilicho chao kwa muda wa miezi miwili?,halafu wakilalamika wanaonekana wakorofi.ni binadamu wachache tu wanaoweza fanya kazi bila malipo na wakachekelea .
 
naomba serikali ibadili jina kutoka dart agency iwe jina jingina maana tunachanganya sana kwa kushindwa kutofautisha kati ya udart na dart
 
Halafu wanasema nchi imepata rais makini hakuna ubabaishaji, huu ni nini?! mtu afanye kazi miezi miwili bila malipo halafu mtu anajitapa jukwaani ni kiongozi wa wanyonge na maskini?! Hawaangalii kwa vitendo amefanya ni wa kulumangia kama kachumbari, hovyo kweli na WAGOME KABISA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…