Watumishi hewa: Kompyuta yenye rekodi yaibwa, wakopa benki kwa majina hewa

Daa hivi watendaji wote wa serikali awamu 4 wanajisikiaje? Mwigulu nae aliwahi kujisifia kuwa atakomesha wafanyakazi hewa akiwa naibu waziri! Sikumuelewa aliposema amedhibiti!! JK alikuwa rahisi kuliko Rais!
Ni upuuzi na chuki kudhani kuwa wafanyakazi hewa wameanza awamu ya nne, labda kama una lako jambo
 
mnao washambulia chadema,hvi chadema ndyo chama tawala nchi hii?uozo mlete wenyewe af saiz mjifanye mnasafisha? Ccm na utawala wenu bado wapuuzi tu,kesi zote mahakamani mnashindwa labda mtu huyo awe upinzani ila nyingne zote mnaburuzwa na mnalipa,hyo inaonyesha kiasi gan mlivyo na mawakili vilaza
 
mchaga wa zanzibar hilo tumekibaini na sasa tunataka kuchukua mawakili binafsi vijana tuwaajiri waifanyie kazi serikali,hatuendekezi tena huu ujinga wa kuchukua waliokosa kazi kwengine ndo kuwapa uhakimu na state Attorney,

Masaju na Mganga wameskia
 
Naanza kufahu asili ya wafanyakazi wa namna hiyo bila shaka familia zao zinafahamu tabia za watoto wao. Kwa maana "like father like son" Basi sasa wanguhofu hata Mungu kama waliona hakuna wakuwahoji. Mzazi kuwa makini na mtoto mramba sukari nyumbani bila shaka huyo ndiye fisadi wa kesho. Maana hata hawa walianzia huko lkn sasa wamehamia hapo walipo. Kwa macho yao hawaoni kama wameiba ndo maana hata utawasikia wakilalamika kuwa wameonewa. Mnh!
 
Pana ombwe la uelewa hapa. Kompyuta ya EPICOR ni maalum kwa kufanyia malipo ya halmashauri au Wizara. Hii inakuwa chini ya wahasibu wakuu wa maeneo hayo.

Kazi ya mtandao wa EPICOR hauingiliani na mtandao wa LAWSON ambao upo chini ya Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri au wa Wizara.

Mifumo yote hii miwili server zake zipo maeneo tofauti. Kwa ndani, Server ya LAWSON ipo Utumishi Dar. Ukiiba hiyo kompyuta utakuwa hujaiba chichote kuhusu kumbukumbu. Watafunga nyingine na zitakuwepo vilevile.

Hali kadhalika kompyuta za EPICOR server ipo Hazina Dar na TAMISEMI Dodoma.

Panahitajika maelezo zaidi ili tujue wameathirikaje kwa data. Naweza kuwaelewa kama watasema walikuwa wamehifadhi data hizo kwenye hiyo kompyuta nje ya mfumo.

Swali la kujiuliza, hawakuwa na backup kama flash disk? Kuna mengi ya kutaka kujua kuhusu kadhia hiyo.
 
Siasa kitu cha ajabu sn!!;jana useme hv kesho vile!!'chandimu watulie'
 
Pana ombwe la uelewa hapa. Kompyuta ya EPICOR ni maalum kwa kufanyia malipo ya halmashauri au Wizara. Hii inakuwa chini ya wahasibu wakuu wa maeneo hayo.

Kazi ya mtandao wa EPICOR hauingiliani na mtandao wa LAWSON ambao upo chini ya Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri au wa Wizara.

Mifumo yote hii miwili server zake zipo maeneo tofauti. Kwa ndani, Server ya LAWSON ipo Utumishi Dar. Ukiiba hiyo kompyuta utakuwa hujaiba chichote kuhusu kumbukumbu. Watafunga nyingine na zitakuwepo vilevile.

Hali kadhalika kompyuta za EPICOR server ipo Hazina Dar na TAMISEMI Dodoma.

Panahitajika maelezo zaidi ili tujue wameathirikaje kwa data. Naweza kuwaelewa kama watasema walikuwa wamehifadhi data hizo kwenye hiyo kompyuta nje ya mfumo.

Swali la kujiuliza, hawakuwa na backup kama flash disk? Kuna mengi ya kutaka kujua kuhusu kadhia hiyo.
Nakubali maelezo yako ya kitaalamu.

Back up server zipo,hapo wamepata hasara ya hilo li desktop tu
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe, Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uandaaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Kaimu Mhazini wa Halmashauri hiyo, Baraka Munuo alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Mwanza, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.

”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Wakati huo huo, MSAKO ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege. Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
CHANZO: Habarileo

Wewe kijana wewe napo kwenye bluu umekuwa fisadi dah "Nilichangia ada yako ya chuo" Imeniuma sana aisee aaaggrrrr
 
Jamaa wanachekesha sana wao ndiyo walikuwa wasemaji wakuu wa ufisadi eti leo hawauoni ajabu na kweli.
24ada2c76196b38421bb7e35459f6e47.jpg
 
tunataka kuchukua mawakili binafsi vijana tuwaajiri waifanyie kazi serikali
...jaji mfawidhi, hapo inabidi muwe makini. Most of those guys are after money, big money. Unaelewa nacho maanisha.

...Nadhani, mfanye appraisal kwa hao mlionao, mwape kazi amnao waamini. Of course, mtahitaji pia kupata wengine.

nb: i just couldn't ignore this.
 
Wafanyakazi hewa ni kama EPA scandal tu ,fedha zinatolewa kwa watu ambao hawa exist
....Naam. Na fedha za WIZI mwingine (EPA, Tegeta Eskrooo, na nyingine), ZIRUDISHWE pia. Mkakati wa makusudi ufanyike kufanikisha zoezi hili....
 
Zoezi la Wafanyakazi hewa kwa sasa ni kaa la moto kwa viongozi wakuu.

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ambaye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa karibu sana na Rais Magufuli imekuwa kama benchmark kwa Wakuu wa Mikoa hata wale waliokuwa wamezoea business as usual.

Swali la kujiuliza kwa sasa, ina maana wale Wakuu wa Mikoa ambao wamekuwepo tokea kwenye awamu ya nne hawakufahamu kama kulikuwa na wafanyakazi hewa katika Mikoa yao?

Nini kimewabadilisha kiasi kwamba kwa sasa wanaonekana very active kuhakikisha Mikoa yao haina wafanyakazi hewa?

Yanayoibuka katika zoezi hili yanatuambia kuna watumishi ambao walifanya wizi ni sehemu ya majukumu yao kikazi.

Kadri zoezi linavyofanyiwa uchunguzi zaidi ndivyo wafanyakazi hewa wanazidi kuongezeka.

Tutaona na kusikia mengi kwenye hili zoezi la wafanyakazi hewa!
Kaka walijua kama kuna wafanyakazi hewa ila viongozi wengi watanzania wanasubiria kauli au amri kutoka juu au waambiwe cha kufanya
 
Huyo mkuu wa mkoa naye ni problem. Kazi ya upelelezi ni taaluma sio maamri ya ovyo, Je asipoipata baada ya hayo masaa anauwezo wa kumfanya nini OCD? Alitakiwa ampe ushirikiano sio kufokafoka.
 
Huyo mkuu wa mkoa naye ni problem. Kazi ya upelelezi ni taaluma sio maamri ya ovyo, Je asipoipata baada ya hayo masaa anauwezo wa kumfanya nini OCD? Alitakiwa ampe ushirikiano sio kufokafoka.
Mie naoa ingekuwa ni jambo la afya kama angefanya kazi hii kimya kimya. Shoo za kwenye vyombo vya habari za NINI? John,mtoto wa Jeturuda na anayetumia jina la Ukoo wa Mama yake, alikuwa amekwenda wasalimia wajomba zake Bukerebe....
 
Back
Top Bottom