Watumiaji wa Mitandao na Watanzania tumelishwa tango pori kuhusu mtoaji Bastola kwa Nape pale Protea

Una uhakika gani kuwa aliwauliza watu ws system?
Aliweka wazi mawasiliano kati yao.?

Yule dada anajua kucheza na akili za watz
 
Unaitaji akili si nguvu kupambana na mjinga
 
kwa hivi sasa tulivyo na mambo ya digitali, nitaamini, kwani humo humo kuna mambo yanatendeka na si ya kuvumilia na kwa vile wamo katika mfumo hawawezi sema kwa woga walionao, hivyo njia wanayotumia ni hiyo tu, nitakupa mfano mzuri wa epa, richmond, buzwagi, wewe unadhani wapinzani walipata wapi hizo hoja, ina maana zilitoka kwa hao hao wasaidizi wa watawala, na kwa vile wao hawawezi simama wakaliongea na ndio maana walitumia upinzani useme na wanakuwa washapewa proof zote, na ndio maana katika mambo hayo utakuta watawala wanadondokea pua, wewe kwa mtazamo wako unadhani kitendo kile kuna watu walipenda waliopo katika ule mfumo, lakini hawawezi kusema, zaidi ya kumtumia mtu kama huyo
 
Una uhakika gani kuwa aliwauliza watu ws system?
Aliweka wazi mawasiliano kati yao.?

Yule dada anajua kucheza na akili za watz
hapana hapo nitakukatalia, kwa mfumo unavyoenda ni haki kabisa habari zinapenya kwa hao hao walioko katika mfumo, dunia ya sasa ni ya kidijitali mkuu,
 
Post utakua umeandikiwa na lemutuz

Sifa yangu humu siku zote ni kuwa muwazi, mkweli na kutokuwa mnafiki halafu kama haitoshi labda nikusaidie tu kuwa Mimi sipelekeshwi na Mtu au Taasisi yoyote na siku zote nitabaki kuwa ' Neutral ' katika yale ambayo nayaamini na nimegundua pia kuwa yawezekana Wewe ni mgeni kwangu kwani hakuna Mtu ninayemdharau humu na kwingineko kama huyo uliyemtaja hapo juu na upo ushahidi wa kutosha tu humu wa Mimi ' kumchamba ' na bahati nzuri hata yeye mwenyewe analijua hilo. Mwisho niseme tu tena kuwa Watumiaji wa Mitandao na Watanzania kwa 100% tumelishwa tango pori ( tumedanganywa ) juu ya hiyo picha. Wenye akili watanielewa na hata wakati naanzisha huu uzi nilijua kuwa nitapata changamoto mno kutoka kwa ' Team Mghaibuni ' kwani yawezekana amewateka akili zenu na amewaaminisha kiasi kwamba nyie wenyewe mnashindwa hata tu kutumia sehemu ndogo ya akili zenu ' kujiongeza ' na ' kutafakari ' kwa umakini zaidi juu ya taarifa zake.
 

Mbona umekimbia? Leta picha
 

Idara aliyoizoea huyo ' Mghaibuni ' wenu siyo hii ya sasa Mkuu. Sitaki niingie ndani zaidi na naomba niishie hapa tafadhali.
 
Aisee hapa nabishana na mtu aliyefungwa mawazo na mange. Kisa mange kasema basi unakimbilia masuala ya epa,buzwagi hata mtu nje ya system atayajua kwa kirefu,wanasiasa ni zaidi ya uwajuavyo.
 
Kama picha umeona na bado unabisha utakua na matatizo, kwa kuongezea tu ni kwamba huyo unaemtetea alitangulia dodoma sku 2 kabla bashite hajaenda kwenye tume. Na ile picha ya hotel alipost si ya arusha kama alivyowadanganya watu fb bali ni morena hotel dodoma. Hotel moja aliyofikia bashite. So unaweza ona kua kuna vingi najua zaid ya hata huyo wa ughaibuni. Skukataz kubisha
 
usijeshangaa wakiweka ileie iliyopo.

Kweli Mkuu ila watanielewa tu taratibu kwani yawezekana ile sumu ya ' Mghaibuni ' wao imeshawaathiri sana hadi wao wenyewe wanashindwa tu kujiongeza.
 
 
Reactions: km1
Aisee hapa nabishana na mtu aliyefungwa mawazo na mange. Kisa mange kasema basi unakimbilia masuala ya epa,buzwagi hata mtu nje ya system atayajua kwa kirefu,wanasiasa ni zaidi ya uwajuavyo.
numbisa nimekupa mifano tu, hakuna aliyenifunga mawazo umefungwa wewe mawazo kwa kuhisi na mtazamo wako kuwa yule jamaa aliyemuonyesha nape bastola ni robot sio binadamu, usalama wa taifa unawafahamu vizuri wewe au unawasikia tu, hawa jamaa ni wabaya kuliko JW ukiingia kwenye anga zao na pale ilikuwa ni anga zao, yani waone sura tofauti ambayo hawaifahamu, aisee utaiona june july, leo uje useme na wewe kuwa yule sio askari, watz hatujawa mambumbumbu kama unavyofikiria,
 
Mkuu una mwamini sana kimambi na kama unamwamini kwanin usitumie akili yako katika kufanya uchunguzi zaidi maana ukifanya uchunguzi utagundua kweli au si kweli
 

Kweli kabisa Mkuu na kumwelewa GENTAMYCINE unatakiwa uwe na IQ iliyoshiba kisawasawa vinginevyo kila siku utakuwa unanichukia tu humu. Wala haiitaji kuwa na Degree sijui Masters au PhD kuweza kujua kuwa picha zile mbili za Protea na za tunayeaminishwa Herry K. Kisanduku siyo za Mtu mmoja na hata ukizilinganisha tu kimwonekano na kwa jicho la Tatu kabisa la ' Kijasusi ' utapata jibu rahisi sana kuwa siyo mwenyewe. Sipingani na taarifa zingine baadhi za huyo ' Mghaibuni ' ambazo kiukweli alikuwa akizitoa huko nyuma ila naambiwa kuna ' mabadiliko ' makubwa yalipita na kuna ' udukuzi ' wa hali ya juu ulifanyika huko hadi tukaona kuwa hata aliyepo huko sasa ni Bingwa wa IT aliyetukuka kabisa na aliyeshiba ' Kiueledi ' ambapo sasa kuna monitoring ya taarifa na wale ambao walishahisiwa ndivyo sivyo wengi wao sasa wametolewa jikoni. Hiyo taasisi iko makini kuliko mnavyodhani na tuendelee tu kudanganyana humu ' Jamvini ' na kudhani kuwa kila taarifa anayowaleteeni ' Mghaibuni ' wenu ni sahihi na ya kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…