Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 9,284
- 14,800
Kabla vita kuanza mwaka juzi Gaza ilikuwa ndio eneo pekee duniani lililokaliwa na watu wengi zaidi kwa kilomita mraba kuliko eneo lolote duniani.
Baada ya karibu miaka miwili sasa Israel imeharibu eneo lote lililokuwa likitumiwa na wapalestina hao kujilimia kitaalamu mboga mboga ambazo ziliwasaidia pakubwa kujikimu kwa chakula
Pamoja na kuminywa kwenye eneo dogo kiasi hicho pia wamezuiliwa kupata chakula na maji yaliyokuwa yakiingizwa eneo hilo kama msaada kutoka nje ya nchi.
Kibaya zaidi watu wote duniani wameshindwa kuingilia kati kuokoa maisha ya watu idadi hiyo na hata kumlaani anayewafanyia unyama huo.
Watu wazima na watoto wamekuwa wakisongamana kwenye majalala kutafuta chochote chenye harufu ya chakula ili watie tumboni.Miongoni mwa wanaoonekani kwenye majalala ni wale waliokuwa matajiri wakubwa wa Gaza ambao walimiliki biashara kubwa pamoja na majengo ya fakhari.
Watoto wadogo walio chini ya miaka 2 ambao ni muhimu zaidi kula ili wapate makuzi ya kuwafanya wawe watu wazima wenye afya wamekuwa wakinyong'onyea kiafya kutakakopelekea kupungua idadi ya wanaokuwa wakubwa ili waje washike nafasi za wazazi wao.
Kutopatikan kwa faragha huku wao wakiwa ni binadamu kumewakosesha nafasi ya kukutana kimapenzi na kuzailaina zaidi.
Hayo yote yakitokea Marekani imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Israel ili kuzuia yeyote nje ya Gaza kuinua sauti kuwateta watu hao.Hapo jana waziri wa Marekani alikuwa Lebanon kuitaka nchi hiyo iwanyang'anye silaha wapiganaji wa Hizbullah mapema iwezekanavyo.Sambamba na hilo Marekani imekuwa ikiwashambulia Houth mfululizo na imeshatayarisha silaha nzito zaidi kwa nia ya kuleta maangamizi kuliko yaliyotangulia.
Matukio hayo yanakwenda sawa sawa na kile alichokitaja na kukiahidi raisi Trump kama jehanamu kwa watu wa Gaza