Watu wa JamiiForums ni wagumu sana kutoa like

mkuuu au umekua addicted na like zakule insta !! hukuu km hueleweki hata like moja hupewi manake watu wanatarajia mengi ya kujifunza kwako,kama huna yaani unaandika pumba ni ngumu kupewa like,vilevile km meseji zako hazina mashiko pia.
 
Watumiaji wa JamiiForums tujifunze kuwapa watu moyo.

Katika Afrika Mashariki JamiiForums ni jukwaa ambalo naweza kusema ni moto wa kuotea Mbali na hili jukwaa limefikia hapo lilipo kwa sababu ya watu kujitolea.

Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mada za JF wakati mwingine unakuta mada imesomwa na watu 3000 lakini unakuta mtu aliyeleta mada amepata like 1 au hajapata kabisa.

Na nina uhakika waliweka kitufe cha like JF hawakuwa wapumbavu lazima kuna maana. Na ninaomba hiyo maana tuitumie pale inapo stahili.
Nisha like nenepa sasa
 
Mkuu mbona una uchungu na hizo 'Likes'?? Kuna kitu zinakuongezea kweli?? Sanasana zinakufariji tu kwa kujiona nimetoa kitu cha maana watu wakakipenda..

Inaonesha unakosa raha usipopata LIKES hapa JF....
LIKES is not a big deal....cha msingi ni kutoa hoja yako ikapokelewa na watu nao wadau wakatoa hoja zao ukapata kujifunza mengi na kujua mambo mengi yaliyokuwa yakikutatiza..LIKES inakuwa kama 'Kisindikizio au kinogesho' cha hiyo hoja yako baada ya wachangiaji kuisoma na kuielewa

Kaa chini jitafakari upya..!
 
Back
Top Bottom