Watoto Media Library: Tupeane mapendekeza ya filamu, nyimbo au vipindi vinavyofaa kwa burudani, maadili na elimu ya Watoto

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Jun 28, 2024
377
1,012
Katika dunia ya leo, vipindi vingi vya kisasa vinaanza kuingiza maudhui yanayoweza kupotosha maadili, hata kwenye burudani za watoto.

Ni jukumu letu kama wazazi na walezi kuchuja na kuhakikisha tunachagua cartoons, filamu, na miziki ambayo sio tu inaburudisha bali pia inalinda maadili mema na ikibidi kuwaelimisha watoto. Tujadiliane na kushirikiana mawazo ya burudani safi kwa watoto

List Yangu

Cartoons
  • Kirikuu
  • Tom and Jerry
  • Looney Toons

Muvi
  • Baby's day out
  • Shaolin Soccer
  • Mr Bean

Vipindi
  • Mpira
  • Mieleka
I
Tafadhalini toeni mawazo ya ziada
 
Kunakipindi Cha zamani Tbc kilikuwa kinaitwa KILIMANINSESAME aisee ile ni bonge la project nimeitafuta mtandaoni sijaipata naona akili akili wanaibia kidogo maudhui yake
 
Mieleka sio mizuri hasa wakiinga ile mitupio. Kuna cartoon ya zamani ilikua inaitwa SARA ilikua nzuri sana na mafundisho mengi
watoto wa kiume wanapenda action, wameumbwa kufanya zaidi action na ulimwengu wa wanaume ni vitendo zaidi,

Kuangalia mieleka inaleta burudani hutaweza kuelewa kama ni mwanamke
 
ishu yangu ni kua sasa iwapo wanashare TV na watu wZima huon kutakua na vurugu?

labda aseme anawatengea ya kwao kuwa mix lazima wapate exposure ya anavowakinga navyo
awawekee tv chumbani, au anunue tablet...

ila kuwazuia wasione mauzauza haiwezekani aisee
 
Back
Top Bottom