Watanzania wanatakiwa wawe na Hela halali ili uchumi ukue

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,389
38,667
Wanasiasa wetu hata Gavana wa sasa wa Benki Kuu wanasema kuwa maisha Kwa binadamu hayajawahi kuwa rahisi na mepesi.

Lakini wao Kila siku wanataka kubakia madarakani kwa hoja kuwa wapo madarakani kuyafanya maisha ya watanzania yawe rahisi na Bora zaidi ya sasa.

Lakini maisha ya watu hayawezi kuwa rahisi kwenye uchumi ulio nyuma.

Maendeleo hutafsiriwa kwa wingi wa watu kuwa na uwezo wa kujikimu vizuri kwenye maisha yao ya kila siku kwa njia halali.

Hapa Tanzania wanasiasa na baadhi ya walio serikalini wanaonesha kuwa haiwezekani kufanikiwa kiuchumi kwa njia halali.

Matokeo yake karibia asilimia sabini (70%) ya biashara na uchumi wa nchi yetu, upo kwenye sekta isiyo rasmi na isiyofuata misingi ya biashara halali.

Uchumi hauwezi kukuzwa kwa kufuata njia haramu kufanyia biashara na kuendesha uchumi.

Uchumi na matumizi ya pesa havitenganishiki. Kama uchumi unaendeshwa kiharamu, ni sehemu ndogo tu ya watu watakuwa "matajiri" huku sehemu kubwa ya watu wakibakia watumwa wa hao matajiri na wanasiasa mafisadi.
 
watu hatuelewi sekta rasmi za uchumi na zisizo rasmi ni zipi.

wewe kama JF ECONOMIST unawezaje kututoa kwenye dilemma ya hivi vitu viwili?
 
First of all I am not an economist!!

Sekta isiyo rasmi mfano mmojawapo ni wale wanaoitwa "wamachinga" au "wajasiriamali"

Lakini pia sehemu kubwa ya wazalishaji wadogo na kati wengi wao hawajasajiliwa.

Ukitaka kujua Hilo angalia idadi ya biashara au shughuli zilizosajiliwa na zile kiuhalisia zilizoko mtaani.
 
Back
Top Bottom